SARATANI NI NINI

Miili yetu ina chembechembe hai nyingi ambazo huzaliana, hukua, na kufa kwa mpangalio maalum
Chembechembe hizi zinapobadirika na kuanza kuzaliana na kukua katika utaratibu ambao sio wa kawaida ndio zinasababisha saratani.

Chembe chembe za Saratani hufuata mfumo huo usio wa kawaida – zinazaliana haraka zaidi bila mpangilio na kukua kwa haraka zaidi na wakati mwingine kuwa na umbile kubwa zaidi.
Chembechembe hizi za saratani zisipodhibitiwa/zisipotibiwa mapema  zina uwezo wa kusambaa na kuota sehemu nyingine ya mwili wa mhusika –

AINA ZA SARATANI

Saratani ni uvimbe unaojitiokeza mahala popote katika mwili wa binadamu, uvimbe huu hauna maumivu yoyote mwanzoni

Saratani zipo za aina nyingi sana na majina yake hutegemea kiungo kilichougua na aina ya chembechembe hai zilizoshambuliwa

Kiungo chochote chaweza shambuliwa,  mfano

  • Shingo ya mfuko wa kizazi
  •  Matiti
  • Ngozi
  • Koo na njia ya chakula Tumbo, utumbo, kongosho, ini
  • Kibofu cha mkojo na tezi dume
  • Mapafu ,ubongo,macho, mifupa,misuli
  • Matezi hasa kwa watoto
  • Damu
  • N.K.

NINI KINASABAISHA SARATANI / VIASHIRIA HATARISHI

Hakuna sababu moja pekee ambayo husababisa saratani, bali ni mchanganyiko wa vitu vingi vinavyotuzunguka ikiwemo Viumbe hai, Kemikali, na aina ya maisha tunaishi kila siku

        Saratani tofauti zina vyanzo vyake tofauti

Mfano

VISIVYOZUILIKA

Jinsia, umri, uwezekano wa kurithi mionzi ya jua??

VINAVYOZUILIKA

  • Matumizi ya kemikali  au Mionzi
  • Uvutaji wa sigara
  • Maambukizi ya baadhi ya vimelea :virus , bacteria, fangasi
  • Matumizi Makubwa ya  pombe
  • Matumizi ya kemikali na mionzi
  • Ulaji mbovu: mafuta mengi, nyama nyekundu kwa wingi  n.k
  • Kutofanya mazoezi
  • Unene uliokithiri
  • Madawa, sumu ya kuulia wadudu
  • Wasichana kuanza ngono  katika umri mdogo


                DALILI ZA AWALI

  • Kila Saratani huwa na dalili zake kutokana na ilipoanzia
  • Mara nyingi saratani haina maumivu mwanzoni na ni ngumu kugundua hasa kamma iko kwa ndani
  • Uvumbe sehemu yoyote ya mwili
  • Mafindofindo
  • Mabadiliko ya haja kubwa au ndogo
  • Kidonda ambacho hakiponi
  • Damu kutoka bila mpangilio au uchafu usio wa kawaida kutoka sehemu za siri(uke)
  • Shida kumeza au kupumua

                DALILI NYINGINE

  • Sauti inayokwama kwama
  • Kuvimba mdomo kwa watoto
  • Kuvimba tumbo kwa watoto

KUCHELEWA TIBA

  • Mgonjwa asipotibiwa mapema saratani huwa kubwa zaidi, na kufanya kidonda
  • Maumivu makali
  • Kusambaa katika viungo vingine vya mwili hasa:
    • Mapafu – Kukohoa na Maumivu
    • Maini – Kujaa Tumbo, Macho kuwa ya njano na maumivu
    • Mifupa – Maumivu / Kuvunjika ovyo
    • Kupoteza kiungo/Viungo vya mwili

UHAKIKI WA SARATANI

Saratani inahakikiwa kwa njia ya kutoa kinyama au ute wa chembechembe husika na kupimwa katika maabara maalum (PATHOLOGY LABORATORY)

Vipimo vingi vya maabara au Radiologia vinaonyesha tu mabadiriko yenye kuashiria uwezekano na siyo uhakiki.

TIBA YA SARATANI KWA UJUMLA

Tiba za kitaalam zilizohakikishwa ni:

  • Upasuaji
  • Dawa za mshipa/dripu, vidonge
  • Mionzi
  • Tiba ya vichochezi/HOMONI
  • Tiba hizi hutumika kwa mchanganyiko kwa kutegemea aina ya saratani, hatua ya ugonjwa na hali ya kiafya ya mgonjwa.
  • Tiba mpya: targeted & Gene therapy

KUPUNGUZA / KUZUIA UWEZEKANO WA KUPATA SARATANI KWA UJUMLA        

  • EPUKA Viashiria hatarishi  vinavyozuilika (66% ya saratani zinazuilika)
  • Jiepushe na uvutaji wa sigara
  • Epuka unene uliopitiliza
  • Fanya mzoezi mara kwa mara
  • Ulaji bora: epuka matumizi ya mafuta mengi na nyama nyekundu kwa wingi, tumia matunda na mbogamboga kwa wingi
  • Epuka matumizi ya pombe kwa wingi
  • Jikinge na mionzi ya jua, hasa  watu wenye ualbino.
  • Jenga mazoea ya kupima afya mara kwa mara
  • Chanjo kwa saratani zenye chanjo mfano,chanjo ya homa ya ini (HBV) na mlango wa kizazi(HPV)