Waziri wa afya Mhe. Jenista Mhagama ametembelea katika Taasisi ya Saratani Ocean Road kuona utoaji huduma za tiba mionzi

      Comments Off on

Waziri wa afya Mhe. Jenista Mhagama ametembelea katika Taasisi ya Saratani Ocean Road kuona utoaji huduma za tiba mionzi

Waziri wa afya Mhe. Jenista Mhagama ametembelea katika Taasisi ya Saratani Ocean Road kuona utoaji huduma za tiba mionzi zinavyoendelea katika Taasisi kwa wagonjwa wa saratani.

Mh. Mhagama amejionea kukamilika kwa matengenezo ya mashine ya LINAC ambayo ilipata changamoto leo asubuhi na kupongeza uongozi wa Taasisi kwa kuhakikisha mashine inafanya kazi ili kuondoa usumbufu kwa wagonjwa.

Mhe Waziri amepongeza kwa kutengenezwa kwa mashine hiyo moja iliyokuwa inasumbua

Hata hivyo, Mhe. Mhagama ameongea na wagonjwa mbalimbali wanaopata huduma katika Taasisi na kuingeza kuwa, serikali ipo mbioni kuongeza mashine nyingine ya Tiba mionzi ili kuondoa shida zinazotokana na uchache wa mashine.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage ameishukuru serikali kwa kufanya mchakato wa kuongeza mashine nyingine ya Tiba mionzi itakayokuja hivi karibuni kwani wagonjwa wa saratani wamekuwa wengi kuhitaji huduma za tiba mionzi.