Uongozi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road umesema kuwa umejipanga kuwa kitovu cha Tiba utalii Africa</h4>

      Comments Off on

Uongozi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road umesema kuwa umejipanga kuwa kitovu cha Tiba utalii Africa</h4>

Ambapo katika kurahisisha shughuli hiyo wamekutana na wadau wa sekta binafsi kutoka Global Medicare kujadili namna ya kushirikiana katika kuitikia wito wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Global Medicare ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Tiba Utalii, Bw. Abdulmalick Mollel, amesema kuwa tiba utalii ni suala mtambuka linalohitaji ushirikiano mpana ili kufanikishwa.

Bw. Mollel amesisitiza kuwa Taasisi ya Saratani Ocean Road ina vigezo vyote vya kuwa kitovu cha tiba utalii kutokana na kuwa na wigo mpana wa wataalamu, miundombinu, na Teknolojia ya uchunguzi na matibabu ya saratani, si kwa Tanzania pekee bali pia kwa nchi jirani, hivyo ni muhimu kuboresha utoaji huduma, kuleta ubunifu katika huduma, na kutangaza huduma hizo ndani na nje ya nchi.

Bw. Mollel pia amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt. Diwani Msemo, kwa kasi yake ya utekelezaji na maboresho makubwa ya miundombinu na huduma, ambayo yamepewa kipaumbele katika Mpango Mkakati wa 2025–2030, ambapo Taasisi inalenga kupata ithibati za kimataifa kwa huduma zake za Vipimo na matibabu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. Diwani Msemo, amemshukuru Bw. Mollel kwa utayari wake wa kushirikiana na Taasisi katika kuandaa mpango mkakati wa tiba utalii ambao utaongeza idadi ya wagonjwa kutoka nje. Katika mwaka 2024, kwani zaidi ya wagonjwa 384 kutoka Zambia, Malawi, Comoro, Kenya, Msumbiji na Burundi walipata huduma katika Taasisi hiyo.

Dkt. Msemo amesema Mpango mkakati unaoandaliwa unalenga kuitikia wito wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kuimarisha tiba utalii nchini.

Dkt. Msemo amesisitiza kuwa menejimenti na wafanyakazi wa Taasisi wanapaswa kuwa tayari kubadili mitazamo yao, kujifunza, na kushirikiana na wenzao wenye uzoefu kutoka sekta binafsi na serikali katika tiba utalii.

Ajenda ya kukuza tiba utalii nchini Tanzania imeanzishwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, na ni miongoni mwa Vipaumbele vya Taasisi hii.