Waziri wa Afya Mhe Mohammed Mchengerwa mapema leo tarehe 02/02/2026 amezindua rasmi matumizi ya mashine aina ya PET CT – Scan ambapo pamoja na uzinduzi huo, ameshuhudia mgonjwa wa kwanza baada ya uzinduzi wa mashine hiyo.


Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Mchengerwa amesisitiza kuwa anatamani kuona mashine hizi zinatunzwa na kuenziwa kwani ndio nembo pekee za maendeleo kwenye sekta ya Afya.
Mhe. Mchengerwa amesema kuwa uwepo wa mashine hii ya PET CT – Scan nchini kwetu utaokoa pesa nyingi sana kwani safari za kwenda India kufuata mashine hii, zilikuwa zikiwagharimu watanzania kiasi cha shilingi milioni 6 mpaka milioni 8, lakini kwa hapa ORCI itakuhitaji kuwa na shilingi milioni moja na laki mbili tu ili kuweza kupata huduma hii kwa haraka huku ikitolewa kwa kiwango cha kimataifa sawasawa na nchi zilizoendelea.
Aidha amewataka watumishi wa ORCI na watanzania kwa ujumla kuendelea kuiamini serikali yao na wakiwa kama wasomi waishike nchi yao kuendeleza uzalendo ili serikali iweze kutulia na kufanya mambo makubwa zaidi ya hayo.
Katika hatua nyingine Mhe. Mchengerwa amempongeza mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa kasi kubwa ya maendeleo anayoifaya na kuongeza kuwa ORCI ndio Taasisi ya kwanza kwa Taasisi zote za kiafya nchini, kutekeleza maagizo yote aliyoyatoa kwa Asilimia Mia moja.






Nae Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Diwani Msemo, amemshukuru Mhe. Mchengerwa kwa kutambua juhudi kubwa ambazo Taasisi hiyo inazifanya katika kuboresha huduma za Afya nchini hususan kwa wagonjwa wa Saratani nchini huku akiahidi kufanya mambo makubwa zaidi ili kuleta mabadiliko ambayo hayakuwahi kutokea nchini Tanzania kwenye sekta ya Afya.
+255-2127597

Waziri wa Afya Mhe Mohammed Mchengerwa mapema leo tarehe 02/02/2026 amezindua rasmi matumizi ya mashine aina ya PET CT – Scan ambapo pamoja na uzinduzi huo, ameshuhudia mgonjwa wa kwanza baada ya uzinduzi wa mashine hiyo.