Rais wa umoja wa visiwa vya Comoro Bw. Azali Assoumani ametembelea kambi maalum ya madaktari bingwa iliyofika katika mji wa Anjouan na kuzungumza na madaktari

      Comments Off on

Rais wa umoja wa visiwa vya Comoro Bw. Azali Assoumani ametembelea kambi maalum ya madaktari bingwa iliyofika katika mji wa Anjouan na kuzungumza na madaktari

Mapema Leo Rais wa umoja wa visiwa vya Comoro Bw. Azali Assoumani ametembelea kambi maalum ya madaktari bingwa iliyofika katika mji wa Anjouan na kuzungumza na madaktari hao.

Akizungumza mara
baada ya kukutana na madaktari hao, Bw. Assoumani amesema uwepo wa madaktari hao ni fursa kubwa kwa wananchi wake hivyo amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo kwani hutokea mara chache kuwakuta wataalam kutoka hospitali mbalimbali wakiwa pamoja.

Bw. Assoumani ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha madaktari hao kutoa huduma, bila malipo yoyote.

Aidha Bw. Assoumani amesema kuwa serikali yake ipo tayari kutoa ushirikiano wa aina yoyote utakaotakiwa na madaktari hao ili mradi waweze kukamilisha kile ambacho kimewaleta hapa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt Diwani Msemo amemshukuru Bw. Assoumani kwa kuweza kufika katika kambi hiyo na kumuhakikishia kuwa hakuna mgonjwa hata mmoja wa Saratani atakaeachwa bila kupata huduma hata ikibidi kuchelewa kuondoka ili kukamilisha hayo.

Aidha Dkt. Msemo amemzawadia Bw. Assoumani Mgolole wa kimasai kama kielelezo cha ushujaa kwa kuchagua kusaidia wananchi wake kwa kukubali ujio wa kambi hii katika nchi yake huku akionesha ushirikiano wa hali ya juu kabisa.

Picha ya pili inaonesha Rais Assoumani katikati (mwenye suti ya bluu na miwani meusi) kushoto kwake ni Gavana wa kisiwa cha Anjoun akifuatiwa na Balozi wa Tanzania Comoro Mheshimiwa Saidi Yakubu pamoja na Dkt. Diwani Msemo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Kulia kwake ni Dr Peter Kisenge Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI pamoja na Dr Asha Mahita ambae ndie mratibu tiba utalii kutoka wizara ya Afya