Date: 08/03/2019
Location: Mlimani City
Wafanyakazi wa jinsia ya kike katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, wameungana na wanawake wote duniani katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani. Siku hii huadhimishwa kila ifikapo tarehe 08/03/ ya kila mwaka. kampeni za siku ya wanawake duniani kwa mwaka 2019, imechagua kuangalizia usawa wenye manufaa ambao unawahamasisha watu duniani kote kuchukua hatua katika kuweka usawa wa kijinsia. Taasisi ya Saratani ya Ocean Road inawatakia, kina mama wote siku njema ya amani na furaha, na kuwahimiza kuwahi mapema katika kufanyiwa uchunguzi wa Saratani.