Wafanyakazi wa benki ya NMB wachangia damu ORCI

      Comments Off on Wafanyakazi wa benki ya NMB wachangia damu ORCI

Wafanyakazi 200 wa benki ya NMB wametekeleza kwa vitendo sera ya kushirikiana na kuhudumia Jamii (CSR), kwa kuchangia damu tarehe 19/10/2019 kwa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road yenye ujazo wa lita 97. Malengo yalikuwa ni kupata damu yenye ujazo wa lita 50, hivyo uchangiaji wa wafanyakazi hao wa NMB ulifanikiwa kuvuka lengo.

Wafanyakazi hao wakiongozwa na meneja wa kanda ya Dar es Salaam ndugu Badru Issa, aliyetoa ujumbe kwa niaba ya benki ya NMB Kwenda kwa wananchi wote wa Tanzania, kuwa, tuna jukumu la kuokoa Maisha ya wagonjwa wetu wa Saratani kwa kuchangia damu, kwani tone moja la damu linachangia katika kuboresha afya ya mgonjwa.

Hospitali ya Saratani ya Ocean Road ikiongozwa na Mkurugenzi wa tiba, ndugu Mark Mseti Pamoja na meneja wa maabara ndugu Samweli Mhina, walitoa pongezi za dhati kwa benki ya NMB kwa moyowa kujitolea na namna walivyoonesha kujali wagonjwa wa Saratani. Pia walitoa wito kwa wananchi wengine kutoka makampuni na au vikundi binafsi, kuwa na moyo kama huo wa kujitolea damu hapa ORCI au popote ilipo benki ya damu salama. Kwani manufaa yanawagusa wagonjwa tofauti tofauti waliopo hospitali zote Tanzania nzima.