Mganga Mkuu wa Serikari aongoza Mashujaa wa Saratani

      Comments Off on

Mganga Mkuu wa Serikari aongoza Mashujaa wa Saratani

Mganga mkuu wa Serikari Dr Aifello Sichwale mapema mwishoni mwa wiki hii ameongoza mamia ya wadau na wahanga mbalimbali katika matembezi ya hisani ya kuhimiza watanzania na watu wote kupima mapema Saratani na kupata matibabu ili kuepuka madhara zaidi ya kuchelewa kupata huduma.

Akizungumza katika maadhimisho ya matembezi hayo yaliyoanzia katika Taasisi ya Saratani Ocean Road Dr Sichwale amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa kupima Saratani kwani inapogundulika mapema inakusaidia kupata matibabu ya haraka na kuepukana na vifo visivyotarajiwa, hivyo amewataka watanzania kufanya hivyo mapema sana ili kupata nafuu hiyo.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dr. Mwaiselage amesema kuwa wanaishukuru sana Serikali kwa kuweza kufanikisha upatikanaji wa Dawa ambapo wananchi wengi wamekuwa wakipata tiba sahihi inayostahili.

Aidha Dr. Mwaiselage amewaasa watanzania kutoogopa kuja kupima kwa kuhofia kipato kwani upimaji huu ni bure na pia kwa upande wa Matibabu wamekuwa wakiwasaidia wananchi kulipa baadhi ya Matibabu hayo kupitia kitengo cha Ustawi wa Jamii ambapo Wananchi hufika hapo na kusaidiwa baadhi ya gharama hizo.

Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka ili kuweza kutoa msisitizo kwa wananchi kuweza kupata vipimo mapema ili kujua Afya zao na km itatokea wamegundulika na Saratani waweze kupata matibabu ili kuepuka madhara makubwa ambayo mwisho wa siku hupelekea vifo.