Naibu waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Doto Biteko amezindua mpango kazi wa Taifa wa haki na ustawi wa watu wenye Ualbino (MTHUWWU)

      Comments Off on

Naibu waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Doto Biteko amezindua mpango kazi wa Taifa wa haki na ustawi wa watu wenye Ualbino (MTHUWWU)

Naibu waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Doto Biteko amezindua mpango kazi wa Taifa wa haki na ustawi wa watu wenye Ualbino (MTHUWWU) na mkakati wa Taifa wa Teknolojia saidizi.

Akizungumza katika maadhimisho ya kilele cha siku ya watu wenye ulemavu nchini, yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond jubilee uliopo Upanga jijini Dar es salaam, Dkt.Biteko amesema kuwa, mpango huu uliozinduliwa naye, ni muhimu kufuatiliwa na kuhakikisha umefanikiwa kwani watu wote nchini ni walemavu watarajiwa na hatujui lini tutapatwa na madhila hayo.

Dkt. Biteko amewaagiza wakuu wa mikoa yote nchini kuhakikisha kuwa wanasimamia maagizo hayo katika maeneo yao ya kazi kwani kwa upande wao ni rahisi mno kwakuwa wapo karibu sana na jamii.

Taasisi ya Saratani Ocean Road nayo imeshiriki katika shughuli hiyo kama mdau mkubwa wa watu wenye Ualbino ambapo imetoa mafuta kwa watu wenye ualbino waliobahatika kutembelea katika banda letu huku wakitoa elimu mbalimbali pamoja na vipeperushi ili kuwapa watu nafasi ya kujifunza mambo mengi kuhusu ualbino

Dkt. Maguha Stephano ambae ni meneja wa huduma za kinga katika Taasisi ya Saratani Ocean Road amesema kuwa mafuta hayo yametolewa bila malipo yoyote huku akiendelea kuwaasa wananchi kusogea katika banda hilo ili kujipatia mafuta hayo pamoja na kujifunza mambo mengine mengi yanayohusiana na saratani pamoja na ualbino.