CHAMA CHA WANAFUNZI CHA WAFAMASIA TANZANIA (TAPSA) CHAPTER YA MUHAS, JANA MAPEMA WAMEZINDUA KAMPENI YA UELIMISHAJI KUHUSU KANSA YA MLANGO WA KIZAZI

      Comments Off on

CHAMA CHA WANAFUNZI CHA WAFAMASIA TANZANIA (TAPSA) CHAPTER YA MUHAS, JANA MAPEMA WAMEZINDUA KAMPENI YA UELIMISHAJI KUHUSU KANSA YA MLANGO WA KIZAZI

Chama cha wanafunzi cha wafamasia Tanzania (TAPSA) chapter ya MUHAS, jana mapema wamezindua kampeni ya uelimishaji kuhusu kansa ya mlango wa kizazi. Katika warsha hiyo ambayo wameuzulia wanafunzi mbalimbali kutoka katika vyuo tofauti vya wafamasia.

Dkt. Kandali Samweli wa Taasisi ya Saratani Ocean Road katika warsha hiyo ya uzinduzi wa kampeni ya uelimishaji kuhusu kansa ya mlango wakizazi amesema, Saratani ya Mlango wakizazi inashika nafasi ya nne Duniani, lakini kwa Tanzania saratani hii inaongoza kwa kushika nafasi ya kwanza.

Dkt.Kandali amesema kuwa katika mapambano ya Saratani hii, Mambo muhimu ya kufanyia kazi ni kujikita katika kufanya uchunguzi wa mara kwa mara na kuwapatia kinga mabinti. Hususani Kinga ambayo hivi karibuni itazinduliwa kwa ajili ya mabinti wenye umri wa miaka 15 mpaka 26.

Aidha Dkt. Kandali amesisitiza kuwa katika kufanya uchunguzi, kama tatizo likigundulika mapema, nafasi ya kupona ni kubwa zaidi kwa kupatiwa matibabu sahihi.

Ata hivyo Dkt. Kandali amesema kuwa, kutokana sababu mbalimbali zinazosababisha Saratani hii, ngono isiyo salama bado inasimama katika nafasi kubwa ya kupata kirusi hicho Cha Papilloma chenye kuleta Saratani hii ya Mlango wa kizazi.

Hata hivyo Dkt. amesisitiza kuwa Dalili za saratani ya Mlango wa kizazi za awali zipo kimya. Kufanya uchunguzi ndio njia pekee ya kuona hizo Dalili za awali zipo au hazipo. Kama zipo unatibiwa kabla ya Saratani kuanza.

Dkt. Kandali amewaasa wanafunzi wawe mabalozi katika kuwafikishia habari hizi watanzania kuwa uchunguzi unaokoa maisha na Saratani inatibika.

Aidha Mtaalamu wa Tiba mionzi Polikalipo Kagina wa Taasisi ya Saratani Ocean Road amewatoa hofu wanafunzi, kuwa mionzi ni salama kwa kuwa inatumika kwa kiwango maalumu pale palipoathirika tu. Na Tiba mionzi haipunguzi siku ya kuishi.
Kagina ameeleza kuwa, mpaka mgonjwa kuanza kupata Tiba ya mionzi huwa anapitiwa na wataalamu Saba mpaka nane ndipo maamuzi ya Tiba mionzi yanafanyika kwa mgonjwa. Na kila mgonjwa ana kiwango chake Cha mionzi kutokana na tatizo lake.

Halikadhalika Mashujaa wa Saratani ya Mlango wa kizazi Bi Asha Juto na Bi Catherine Bachoo kwa pamoja wamesema kuwa wamepona Saratani na wanaendelea na maisha yao Kama kawaida. Na wamekuwa wakitoa Elimu kuhusiana na Saratani hii ya Mlango wa kizazi.