Mambo makubwa manne kwa siku ya leo toka kwa mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. JuliusMwaiselage.
- Shukrani kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha matibabu kwa kutuletea vifaa tiba vya kutosha kwaajili ya watanzania.
- Bima ya Afya kwa wote itasaidia wananchi kuweza kupata matibabu kwa urahisi, hivyo pindi itakapopitishwa tu tuharakishe kujiunga ili kuokoa maisha ya watanzania hasa wa hali ya chini
- Siku ya kuadhimisha mapambano dhidi ya Saratani, watanzania wahakikishe wanapata taarifa sahihi kuhusu Saratani.
- Shukrani kwa CRDB kwa kutusaidia kuhusu kupata kituo cha mawasiliano cha hudu.a kwa mteja, hii itasaidia kutoa taarifa sahihi kwa watanzania kuhusu huduma zetu za saratani.