Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, inapenda kuwaarifu wananchi wa Tanzania kuwa, huduma za kisasa za uchunguzi wa Saratani ya matiti kwa machine ya mammogram imerejea.
Uchunguzi kwa kutumia mammography ni njia mahsusi ya upimaji wa titi unaotumia dozi ndogo ya X RAY kutambua uwepo wa saratani mapema kaba ya mwanamama hajaanza kuonesha dalili nyengine. Uchunguzi huu huwa ni wa mapema na husaidia Zaidi katika kutibu saratani ya matiti.