ORCI YAANZISHA HUDUMA YA KUTUMIA MIONZI YA IMRT

      Comments Off on ORCI YAANZISHA HUDUMA YA KUTUMIA MIONZI YA IMRT

TAASISI ya  Saratani ya Ocean Road (ORCI) imeanzisha huduma mpya ya kibingwa ya kutibu ugonjwa wa saratani kwa miale ya mionzi kwa njia ya  kisasa zaidi ijulikanayo kama Intensity  Modulated Radiation Therapy (IMRT), ambapo tiba yake ni ya mionzi ikiwa inatibu  eneo mahususi  yenye tatizo pekee.

Tanzania inakuwa ya kwanza kutumia huduma hiyo ya IMRT kwa ukanda huu wa Afrika  Mashariki huku kwa Afrika inaingia kuwa nchi ya tatu baada ya Afrika Kusini na Misri.

Kwa mataifa mengine huduma hiyo inatolewa kwa nchi za Marekani na India pamoja na baadhi ya nchi ya za Ulaya.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mtendaji wa ORCI, Dk. Julius Mwaiselage, alisema kwa sasa wagonjwa waliokuwa wakienda kutibiwa Nchini  India watakaporejea wataweza kutibiwa hapahapa kwa sasa kwani tayari wamenzisha huduma hiyo.

‘Huduma hii awali ilikuwa inapatikana nje ya nchi haswa nchi zilizoendelea ikiwe, India. Hivyo hata wagonjwa watakaporejea  hapa nchini wataweza kupata tiba hii hapa hapa  na wakaendelea na matibabu.

“Awali tulikuwa tunatoa tiba ya teknolojia ya 3D ambapo kwa sasa tumeziongezea uwezo yaani kuzimobireti na kuja na huduma hii mpya kwa kutumia mashine hizi hizi za ‘LINAC ACCELERATOR.’ Alisema Mwaiselage.

Dk. Mwaiselage amesema mashine hizo zimenunuliwa  kwa fedha za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dk. John Pombe Joseph  Magufuli zikiwa mpya kabisa kutoka kiwandani kwa TSh. bilioni 9.5  zikiwa mbili  ya mionzi na ya kupanga tiba, mwaka 2018 na kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan mwaka 2019 ambapo imekuwa na uwezo wa kutoa  tiba mbalimbali za mionzi ikiwemo teknolojia ya 3D na zingine zikiwemo ya tiba ya upasuaji wa mionzi na zinginezo.

‘Toka zimefka hizi mashine tulianza na hii ya mionzi kwa teknolojia  ya 3D, lakini kwa sasa mashine hizi tumezi ongezea  uwezo ‘upgrade’  na  kuanza kutumia tiba hiyo ya kisasa zaidi ya IRMT ambayo kwa sasa inatumika Duniani kote ikiwemo Afrika Kusini, Lakini India na Marekani.

Tiba hii ni mahususi kabisa kwa kutibu maeneo yale ambayo ungeona hauitaji kufikiwa n miale ya mionzi mikali kwenye eneo ambalo usingetaka iguswe.

Kwa upande wake Daktari bingwa wa Saratani wa ORCI, Dk.Sikudhani  Muya alisema kuwa tiba hii mpya ni maalum ambapo itasaidia kuzuia mionzi mikali kuzuiwa isipenye maeneo mengine isidhurike.

‘Huduma hii inasaidia kutibu eneo lenye saratani  kwa miale yake ya mionzi kuenda kutibu eneo lile pekee lenye tatizo. Mfano  uvimbe wa saratani ukiwa eneo la kichwa basi tiba hii mionzi yake itaenda kutibu tu eneo hilo na sehemu za ubongo hazitaguswa. 

Hii ndio faida kuu ya tiba hii na ni ya kipekee sana ambapo inachukua dakika kuanzia 10 hadi 30.’ Alisema Dk. Muya.