MAWASILIANO BAINA YA WATOA HUDUMA ZA AFYA NI MUHIMU KATIKA KUPATA VIPIMO SAHIHI VYA MGONJWA.

      Comments Off on

MAWASILIANO BAINA YA WATOA HUDUMA ZA AFYA NI MUHIMU KATIKA KUPATA VIPIMO SAHIHI VYA MGONJWA.

Mtaalamu wa Maabara wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Bw. Peter Mwevila amesema swala la mawasiliano baina ya watoa huduma za afya ni muhimu katika kupata vipimo sahihi vya mgonjwa.

Bw. Mwavila ameyasema hayo leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo katika majengo ya Taasisi ya Saratani Ocean Road alipokuwa akiwasilisha mada inayosema “Sample Collection” katika uwasilishaji wa “Continues Medical Education” (CME).

Aidha Bw. Mwevila ameongeza kuwa katika uchukuaji wa “sample” kutoka kwa mgonjwa ni lazima kuzingatia maelekezo ya kila kipimo kinachohitajika kwa kuwa kila kipimo kina utaratibu wake.

Pamoja na hayo Bw. Mwevila ameongeza kuwa iwapo sample imecheleweshwa kufikishwa kwenye maabara au “sample” imehifadhiwa katika kifaa kisicho sahihi, itabidi kuchukuliwa “sample” nyingine ili kupata vipimo hitajika.

Taasisi ya Saratani Ocean Road imekuwa ikitoa fursa kwa idara na vitengo vya ndani na nje ya Taasisi katika kuwasilisha mada mbalimbali kwa watumishi wake, ili waweze kujenga uelewa wa pamoja.