SERIKALI YAIMARISHA HUDUMA ZA MATIBABU YA NYUKLIA

      Comments Off on

SERIKALI YAIMARISHA HUDUMA ZA MATIBABU YA NYUKLIA

SERIKALI YAIMARISHA HUDUMA ZA MATIBABU YA NYUKLIA – DKT UBUGUYU.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania inayoongozwa na Mhe Dk.Samia Suluhu Hassan imeimarisha huduma za matibabu yuklia yakihusisha uchunguzi na tiba hasa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kutoka Wizara ya Afya, Dkt Omary Ubuguyu, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika ufungzi wa mafunzo ya wataalamu wa tiba nyuklia kutoka nchi 15 barani Afrika yanayofanyika katika Taasisi ya Saratani Ocean Road.

Akizungumza zaidi Dkt Ubuguyu amesema Serikali imeanza kuongeza uwezo katika kuimarisha teknolojia za kisasa katika uchunguzi na tiba magonjwa ya saratani nchini ikiwemo ununuzi wa mashine ya kisasa ya uchunguzi na tiba ya PET/CT scan katika Taasisi ya Saratani Ocean Road. Aidha mashine za awali zipo katika hospitali Bugando na Taasisi ya Saratani Ocean Road

Aidha, alieleza jitihada zaidi za Serikali ya Tanzania katika maandalizi ya kujenga kituo cha umahiri wa matibabu ya saratani nchini ambacho kitakuwa bora kuliko vyote Afrika.

Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka kipaumbele suala la kuboresha matibabu ya kansa katika Taasisi hiyo kwa kutoa fedha za kujenga miundombinu mbalimbali na kununua mashine mbalimbali za matibabu na vifaa tiba.

Dkt Mwaiselage, amesema kuwa mafunzo haya ya watalaamu yamefanyika kwa usimamizi wa Shirika la Nguvu za Atomu Duniani (IAEA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani Ocean Road, na kwamba IAEA inaitambua Taasisi kwa umahiri wake ndiyo maana mafunzo ya Afrika yanaletwa kufanyika katika Taasisi.

Nae daktari Bingwa wa Magonjwa ya Nyuklia wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. Tausi Maftah, amesema kupitia Teknolojia hiyo wanafanya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ikiwemo Figo, Moyo, mifupa, na magonjwa ya njia ya chakula kwa kutumia Nyuklia isiyo na athari kwa binadamu kwa makundi mbalimbali wakiwemo watoto.

Alisema kuwa huduma hiyo ya matibabu nyuklia inq changamoto kubwa sana nchini kwetu hivyo mafunzo haya yatachochea uelewa na kuboresh huduma za matibabu