TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD YAENDELEA NA HUDUMA KATIKA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA KIBIASHARA(SABASABA)

      Comments Off on

TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD YAENDELEA NA HUDUMA KATIKA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA KIBIASHARA(SABASABA)

Taasisi ya Saratani Ocean Road imeendelea na utoaji wa huduma za uchunguzi wa awali kwa Saratani ya Mlango wa Kizazi, Tezi Dume, Saratani ya Matiti na ile ya ngozi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) katika mabanda yao yaliyopo ndani ya viwanja vya maonesho ya biashara ya kimataifa vya Sabasaba.Akizungumzia kuhusu

Uchunguzi huo kaimu mkurugenzi wa kinga Dr. Maguha Stephano amesema kuwa uchunguzi huo unafanyika bila malipo yoyote yale, hivyo amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kupima Afya zao.

Aidha Dr. Stephano amesema kuwa pamoja na uchunguzi huo pia wanatoa huduma ya upimaji wa homa ya Ini pamoja chanjo yake, pia huduma ya chanjo ya UVIKO-19 ipo.

Dr. Stephano amesisitiza wananchi kutembelea banda hilo na kupata elimu kuhusu ugonjwa wa Saratani kwani ugonjwa huu ni hatari kuliko baadhi ya magonjwa yanayodhaniwa ni hatari ila kwakuwa bado elimu haijawafikia wanaudharau.

“Naendelea kusisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika banda letu ili kuweza kupata elimu sahihi ya ugonjwa huu, kwani ugonjwa huu ni hatari sana ukilinganisha  na baadhi ya magonjwa ambayo hudhaniwa hatari na kuudharau ugonjwa huu kutokana na kukosa elimu juu ya uhatari wake”. Alisema Dr. Stephano.