HONGERENI KWA KUTOA CHANJO YA UVIKO-19 ILA ONGEZENI HAMASA- WAZIRI UMMY MWALIMU

      Comments Off on

HONGERENI KWA KUTOA CHANJO YA UVIKO-19 ILA ONGEZENI HAMASA- WAZIRI UMMY MWALIMU

Waziri wa Afya Mh. Ummy mwalimu ameipongeza Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa kuamua kuhamasisha watu kupata chanjo ya UVIKO-19 

Akizungumza ndani ya viwanja vya maonesho ya kimataifa ya kibiashara alipotembelea  katika banda la Taasisi ya Saratani Ocean Road waziri Mwalimu amesema kuwa Taasisi hiyo imejitahidi sana kwenye utoaji wa chanjo hiyo huku akisema kuwa idadi iliyotajwa kwa watu waliopewa chanjo hiyo bado ni ndogo hivyo kuwaasa waongeze nguvu ili kuweza kupata idadi kubwa zaidi.

Awali akitoa wasilisho la Taasisi Afisa mawasiliano na uhusiano wa Taasisi hiyo Bw. Islam Mposso amesema kuwa mpaka muda ambao Mh. Mwalimu anapita tayar watu zaidi ya 34 walikwishapatiwa chanjo ya UVIKO-19.

Taasisi ya Saratani Ocean Road inashiriki maonesho ya 46 ya kimataifa ya biashara ambapo inatoa huduma za upimaji ws saratani ya Tezi Dume, Matiti, Ngozi ka watu wenye Ualbino, Mlango wa kizazi kwa wakina mama, hata hivyo inatoa pia huduma ya upimaji na utoaji chanjo ya homa ya Ini pamoja na UVIKO-19