TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD LEO KATIKA KILELE CHA MAAZIMISHO YA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI IMEPOKEA MISAADA MBALIMBALI KUTOKA KWA WANAWAKE WA TAASISI NA IDARA MBALIMBALI

      Comments Off on

TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD LEO KATIKA KILELE CHA MAAZIMISHO YA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI IMEPOKEA MISAADA MBALIMBALI KUTOKA KWA WANAWAKE WA TAASISI NA IDARA MBALIMBALI

Taasisi ya Saratani Ocean Road leo katika kilele Cha maazimisho ya siku ya Mwanamke Duniani imepokea misaada mbalimbali kutoka kwa wanawake wa Taasisi na idara tofauti tofauti hapa nchini Tanzania kwa ajili ya wagonjwa.

Msimamizi wa Kitengo cha Ustawi wa Jamii wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Bi. Devotha Kovaga amesema wanawake wameleta misaada tofauti tofauti ikiwemo viti vya kuwabebea wagonjwa, Sabuni, Dawa za meno, pesa taslimu kwa baadhi ya wagonjwa na vitu vingine vidogo vidogo vya kuwasaidia wagonjwa katika mahitaji yao. Pia wakina mama hao wamewanunulia wagonjwa dawa kwa wale ambao siku ya Leo wamekuwa na changamoto ya kugharamia dawa.

Aidha Bi. Kovaga amesema makundi ya wanawake hao ni wanawake kutoka Benki ya Maendeleo ya kilimo (TADB), wanawake kutoka kampuni ya Said Salim Bakhresa Co. Ltd, wanawake kutoka Maabara ya Taifa, wanawake kutoka TCRA, wanawake kutoka Airport pamoja na wanawake kutoka Mamlaka ya mapato idara ya walipa Kodi wakubwa.

Pamoja na hayo Bi. Kovaga ametoa shukrani kwa wadau wote waliotoa misaada hiyo na kutoa wito kuwa wagojwa wanaitaji misaada ya mara kwa mara, hivyo wanakaribishwa muda wowote kuja na kutoa misaada.
Na amesisitiza kuwa ugonjwa wa Saratani inatibika, muhimu ni kufanya uchunguzi wa mara kwa mara na kupata tiba sahihi.