MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD, DKT. JULIUS MWAISELAGE, AMEWATAKA WANAWAKE KATIKA TAASISI HIYO KUFANYA KAZI KWA BIDII…

      Comments Off on

MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD, DKT. JULIUS MWAISELAGE, AMEWATAKA WANAWAKE KATIKA TAASISI HIYO KUFANYA KAZI KWA BIDII…

Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. Julius Mwaiselage, amewataka wanawake katika Taasisi hiyo kufanya kazi kwa bidii na kufuata misingi ili kuweza kupata mafanikio zaidi kwenye maisha yao.

Akizungumza wakati akitoa salamu zake za siku ya wanawake Duniani Dkt. Mwaiselage amesema kuwa msingi ulio imara na ambao ndio nguzo thabiti kwenye kila maendeleo ni kufanya kazi kwa juhudi na kufuata misingi kwenye shughuli anayofanya.

Aidha Dkt mwaiselage amewaasa wanawake wa hapa kushirikiana katika kuwasaidia wanawake wengine hasa kwenye tatizo hili la Saratani ya Matiti na mlango wa kizazi ili kuweza kuokoa kina mama wengi ndani na nje ya nchi

Dkt. Mwaiselage amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae ndie amewezesha kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa mashine nyingi za kusaidia uchunguzi ikiwamo mammogram, MRI na mashine nyingine nyingi ambazo zitasaidia kurahisisha uchunguzi wa Saratani katika Taasisi hiyo.

Kila inapofika Tarehe 08/03/ ya kila mwaka, huwa ni siku ya wanawake duniani ambapo wanawake kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road husherehekea kwa namna yake ikiwamo kutoa Jumbe mbalimbali zinazosaidia kinamama kuutambua ugonjwa wa Saratani hususan Saratani ya Mlango wa kizazi na Matiti.