Dkt Mwaiselage akabidhi Makombe kwa bodi ya udhamini.

      Comments Off on

Dkt Mwaiselage akabidhi Makombe kwa bodi ya udhamini.

Dkt Mwaiselage akabidhi Makombe kwa bodi ya udhamini.

Na Mwandishi wetu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt Julius Mwaiselage amekabidhi makombe matatu yaliyopatikana katika mashindano ya MEI MOSI kwa Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini katika Taasisi hiyo Prof. Ephata Kaaya.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Dkt. Mwaiselage amesema kuwa katika Taasisi hii wanamichezo wamekuwa wakijitoa kwa hali na mali ili kuweza kuleta heshima katika Taasisi hii.

Akiendelea Dkt. Mwaiselage amesema kuwa kwa miaka takribani mitatu mfululizo wamekuwa wakirudisha makombe zaidi ya matatu huku wakiitangazq Taasisi kwa ushindi wa wa jumla ambapo kwa mwaka huu wamejinyakuliq ushindi wa tatu kwenye ushindi wa jumla kwa kuvuna point 7.

Nae Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa Taasisi hiyo prof. Ephata kaaya ameupongeza uongozi wa Dkt. Julius Mwaiselage kwa kuendelea kusimamia vyema swala la michezo katika Taasisi pamoja na kazi nyingi na ngumu wanazoendelea kuzifanya.

Akipokea makombe hayo Prof. Kaaya amesema bodi yake ipo tayari kushirikiana na wanamichezo wote na inaendelea kuwatia nguvu zaidi ili wakati mwingine waweze kuleta makombe zaidi ya hayo matatu.

Prof. Kaaya amesisitiza kuwa, wafanyakazi wanapomaliza kazi zao wakumbuke kufanya mazoezi kwaajili ya Afya zao lakini pia kusaidia kusukuma mbele gurudumu la kimichezo kwa Taasisi ili kuweza kujipatia sifa na kuitangaza taasisi kwa shughuli za kimichezo na kimatibabu.