ORCI YATOA SOMO KUHUSU SARATANI KWA WAHUDUMU WA AFYA LINDI.

      Comments Off on

ORCI YATOA SOMO KUHUSU SARATANI KWA WAHUDUMU WA AFYA LINDI.

ORCI YATOA SOMO KUHUSU SARATANI KWA WAHUDUMU WA AFYA LINDI.

Na Mwandishi wetu

Taasisi ya Saratani Ocean Road, leo imetoa somo kuhusu Saratani kwa baadhi ya wahudumu wa Afya kutoka katika hospitali ya Rufaa ya Sokoine.

Akitoa somo hilo kwa kushirikiana na baadhi ya madaktari, Dkt. Maguha Stephano amesema kwa sasa ugonjwa huu umeendelea kuwa hatari kitu kinachofanya Taasisi kuendelea kuwekeza kwa kununua mitambo ya kisasa ili kuweza kusaidia wananchi kulingana na matatizo yao.

Aidha Dkt. Maguha amewaeleza whudumu hao wa Afya kuwa pamoja na uhatari wa Saratani lakini unatibika hivyo amewasisitiza kuwaeleza wagonjwa kuwa waweze kufika kufanya uchunguzi mapema ili ikiwa atagundulika mapema basi aweze kufanyiwa rufaa kufika Taasisi ya Saratani Ocean Road kwaajili ya uchunguzi zaidi na matibabu.

Pia Dkt Maguha amesema kwa watanzania hii ni fursa kubwa kuitumia kwani kama nchi nyingine za Afrika wanaitumia kwa kuweza kuja na kutibiwa kutokana na uwekezaji wa Serikali ya awamu ya Sita inayoongzwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwanini sio wenye nchi yao, hivyo amesisitiza kuitumia fursa hiyo ili kuepukana na hatari inayoweza ikajitokeza.

Taasisi ya Saratani Ocean Road inatekeleza Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuwatembelea wananchi walioko pembezoni na kuwapa huduma hizi bila malipo yoyote, hivyo katika uchunguzi wa hatua za awali kwa mikoa yote ambayo Taasisi itapita itatoa huduma hizi bila malipo yoyote ambapo kwa mwezi huu Taasisi ipo Lindi kwaajili ya kufanya uchunguzi wa Saratani za Matiti, Mlango wa kizazi kwa wakina mama pamoja na Tezi Dume kwa wakina baba na baadae Tarehe 07/05/2023 timu hiyo itaelekea Mtwara kwa kutoa huduma hizo hizo mpaka tarehe 12/05/2023, huku mpango huu ukiwa umewekwa vizuri ili kila mwezi kuwe na mkoa mmoja au miwili ambayo itatembelewa na kupewa huduma hizo.