Ebeneza Women Group wawafariji wagonjwa waliolazwa Ocean Road

      Comments Off on

Ebeneza Women Group wawafariji wagonjwa waliolazwa Ocean Road

Kikundi cha kina-mama ‘Ebeneza Women Group’ kimewatembelea, kuwajulia hali na kuwafariji wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), iliyoko Mkoani hapa.

Mapema leo baadhi ya wanachama wa hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Beatrice Masolwa, wamekabidhi zawadi mbalimbali kwa wagonjwa hao.[15/10, 10:30] Bwana: Akizungumza, Masolwa ametaja baadhi ya zawadi hiyo ‘diapers’ za watu wazima, miswaki, dawa za meno, sabuni za kuoga na kufulia maji na nyinginezo.
“Thamani ya vitu vyote tulivyonunua ni kiasi cha Sh. 500,000,” amebainisha.

Amesema wameguswa kufika hospitalinihapo kuwaona na kuwafariji wagonjwa  kwani ni sehemu ya jamii.[15/10, 10:30] Bwana: Amehimiza jamii kujenga na kuendeleza utamaduni wa kuwatembelea, kuwajulia hali na kuwafariji wagonjwa waliolazwa hospitalini.
“Unapoishi jua kuna mgonjwa aliyelazwa hana ndugu, anahitaji msaada na faraja, sisi ndio wa kwenda, kuwafariji na kuwasaidia chochote tulichojaliwa,” ametoa rai Masolwa.[15/10, 10:30] Bwana: Wanahitaji upendo hasa wakati ambapo wapo wodini wakipatiwa matibabu na wakiendelea kupigania uhai wao,” amesisitiza.
Ameongeza kwamba “Kuna watu wanahitaji kutiwa moyo na sisi tumeona ni watu wenye dhamana hiyo, tukaja kuwatembelea.