Bwana: Majibu ya maabara kwamba amekutwa na saratani ya matiti iliyofikia hatua ya tatu, miaka 11 iliyopita haikuwa rahisi kwa Lucy kuyapokea.
Daktari wake alipomjulisha juu ya majibu hayo, fikira zake ‘zilimsafirisha’ hadi kuanza kutafakari namna mazishi na maziko yake yatakavyokuwa.
Akisimulia mbele ya mashujaa zaidi ya 30 wa saratani {Waliotibiwa na kupona na wanaoendelea na matibabu dhidi ya maradhi hayo}, Taasisi ya Saratani Ocean Road, Lucy amesema alifanyiwa upasuaji na kuondolewa titi lake ili kuokoa maisha.
Mashujaa hao wamekutanishwa leo katika ukumbi wa Nyerere ndani ya taasisi hiyo na Chama cha Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani {TOS} kupewa semina maalum iliyolenga kuwapa uelewa jinsi ya kuishi na kukabiliana na changamoto baada ya kukutwa na magonjwa hayo.
Lucy amesema wagonjwa wa saratani hukumbana na mikasa mingi na ikiwa mtu hana taarifa sahihi wapo ambao huacha matibabu na kukimbilia kwengineko.
Akiendeleza simulizi yake ilivyokuwa siku hiyo alipopewa majibu, amesema alitafakari pia namna gani ataweza kumudu ukurasa mpya wa maisha atakayoishi, akiwa na saratani.
“Ilikuwa 2010, mume alikuwa ameshafariki 2006, Hivyo nilitafakari juu ya watoto wangu waliokuwa na mdogo wakati huo, watabakije bila mama, wala baba.
“Ilinipa wakati mgumu, kiasi cha kushindwa kurejea nyumbani mwenyewe, ilibidi ndugu zangu wanifuate siku hiyo,” amesimulia.
Amesema alijawa na msongo wa mawazo na hilo lilichangiwa na uelewa duni aliokuwa nao kipindi hiçho kuhusu ugonjwa wa saratani.
“Nilikuwa sijui satatani ni nini, nilichokuwa nafahamu, mtu akiugua anakufa, nilijua ni ugonjwa wa watu wengine si wangu yaani sitakaa itokee niambiwe nina saratani.
“Lakini nikakutwa nayo, ilianza uvimbe mdogo na niliouna siku moja nilipoamka asubuhi, sikuwa na maumivu yoyote awali, niliendelea na shughuli zangu,” amesimulia.
Lucy amesema uvimbe uliendelea kukua na maumivu yalianza kubisha hodi, alilazimika kwenda hospitali hatimaye akagundulika kuwa na saratani hiyo.[28/10, 07:56] Bwana: Lucy amewasisitiza mashujaa wenzake wasiogope, wasisikilize taarifa potofu kuhusu saratani na wasiache matibabu kwani inatibika na mtu anapona kabisa kama ilivyokuwa kwake.
“Nimepona na nimezidi kuwa mrembo baada ya matibabu, nimeolewa na wanangu wamekuwa wakubwa maisha yanaendelea kama kawaida,” amesema
Mariam Isaya amesema semina hiyo imemsaidia kujifunza mengi na kumpa ujasiri zaidi kuendelea kupambana dhidi ya saratani ya kizazi aliyokutwa nayo.
Naye, Juma Kassim ameshukuru uongozi wa chama hicho kuandaa semina hiyo, kwani amekutana na mashujaa wenzake imempa imani kwamba hayupo peke yake na ipo siku atapona na kuwa historia.[28/10, 07:57] Bwana:
Akizungumza kwa niaba ya Rais wa TOS, Katibu wa Chama hiyo, Dk. Caroline Swai {pichani} amesema semina hiyo imeandaliwa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yao kuhakikisha jamii inapata uelewa wa kutosha juu ya saratani mbalimbali.
Amesema wagonjwa wa saratani wanakutana na mabadiliko kadhaa kipindi cha matibabu, hivyo ni muhimu kuzidi kuwapa elimu sahihi jinsi gani wataweza kukabiliana nayo.
Amesema elimu inatolewa kwa mbinu mbalimbali pia ikiwamo kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Dk. Jennifer amesema Chama hicho ni kipya kimezinduliwa Novemba, mwaka jana na kwamba kimedhamiria kuifikia jamii hadi vijijini, kuielimisha.[28/10, 07:57] Bwana: Tuna jukumu kuu la kuhakikisha pia zile huduma wanazopewa wagonjwa zinakidhi viwango sawa na vile vinavyofanyika mataifa yaliyoendelea.
“Akitibiwa hapa akienda Marekani akute huduma ni Ile ile, tunayotoa hapa Tanzania. Apate huduma bora, tumejikita nyanja mbalimbali kuhakikisha huduma zinakuwa bora, tunafanya tafiti pia,” amebainisha.