Ilala Afya Center kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani Ocean Road wameendelea kutoa huduma mbalimbali za Afya

      Comments Off on

Ilala Afya Center kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani Ocean Road wameendelea kutoa huduma mbalimbali za Afya

Ilala Afya Center kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani Ocean Road wameendelea kutoa huduma mbalimbali za Afya ikiwamo kupima Saratani mbalimbali katika Hospitali ya wilaya ya wete ndani ya visiwa vya Pemba.


Akizungumza mapema leo Daktari kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dr. Katanga amesema kuwa leo ikiwa ni siku ya pili watu wameendelea kujitokeza kwa wingi kupata huduma mbalimbali za kimatibabu kama upimaji wa Macho, masikio na magonjwa mengine mbalimbali huku upimaji wa Saratani ukishika kasi kubwa kwa kupatikana kwa watu wengi.


Aidha Dr. Katanga ametanabaisha kuwa pamoja na kujitoleza kwa watu wengi katika kampeni hiyo, lakini bado amewasihi wananchi wakaazi wa eneo hilo na walioko pembezoni kuendelea kujitokeza kwani muda bado upo sababu kampeni hii inafanyika kuanzia tarehe10 Agosti mpaka Tarehe 13 Agosti mwaka huu.
Nao wananchi wameishukuru Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa kushirikiana na Ilala Afya center kwa kuweza kuunganisha nguvu ili kuleta matibabu sahihi na mengi kwa ujumla wake kwani mtu akifika hapo anapata vipimo vyote na matibabu yote kwa mpigo na akiondoka anakuwa na uhakika na Afya yake.