MGANGA MKUU WA MANISPAA YA  MPANDA DR. PAUL SWAKALA AMEISHUKURU TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD KWA KUWEZA KUFANYA MAAMUZI YA KUFIKA NA KUWAHUDUMIA KWA VIPIMO WANANCHI NA WAKAAZI WA MANISPAA HIYO.

      Comments Off on

MGANGA MKUU WA MANISPAA YA  MPANDA DR. PAUL SWAKALA AMEISHUKURU TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD KWA KUWEZA KUFANYA MAAMUZI YA KUFIKA NA KUWAHUDUMIA KWA VIPIMO WANANCHI NA WAKAAZI WA MANISPAA HIYO.

Mganga mkuu wa manispaa ya mpanda Dr. Paul Swakala ameishukuru Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa kuweza kufanya maamuzi ya kufika na kuwahudumia kwa vipimo wananchi na wakaazi wa manispaa hiyo.

Akizungumza na wakazi hao waliojitokeza kwa wingi kupima katika viwanja vya Kashato, Dr. Swakala amesema kuwa hivi ni vipimo muhimu sana hasa ukizingatia kuwa Taasisi ya Saratani Ocean Road wamekuja kuwafata wananchi ili waweze kupata huduma hiyo karibu kabisa ili kuwaepushia gharama za kufata huduma hizo Dar es Salaam.

Akiwakumbusha zaidi Dr. Swakala amesema kuwa madaktari waliokuja hapa nimabingwa kabisa hivyo amewataka wanampanda kujitokeza kwa wingi sana ili kuepusha kuwavunja moyo kwani wanahitaji wakati mwingine wafike hapa Mpanda.

Nae mkuu wa msafara wa Madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road na Meneja wa huduma za kinga wa Taasisi hiyo Dr. Maguha Stephano amewashukuru kina baba kwa kujitokeza kwa wingi mno zaidi ya kina mama ili kuweza kupata huduma ya vipimo vya Saratani ya Tezi Dume.

Aidha ameendelea kusisitiza kuwa wananchi wajitokeze zaidi kwani wapo katika kampeni hiyo kwa siku Tatu kuanzia tarehe 18 mpaka 20 Julai ili kuweza kuwasaidia wananchi wengi zaidi huku akisema kuwa huduma zote zitatolewa bure kabisa

“Nasisitiza wananchi kujitokeza kupata vipimo kwa wingi kwani tupo kwenye kampeni hii kwa muda wa siku tatu kuanzia leo jumatatu Tarehe 18 mpaka tarehe 20 mwezi huu, na huduma hii inatolewa bure kabisa hivyo karibuni sana.” Alimaliza Dr. Maguha.

Timu ya Madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, ipo mkoa wa Katavi katika Manispaa ya Mpanda ili kuweza kutoa huduma za upimaji wa aina mbalimbali za Saratani na magonjwa mengine km kisukari, presha n.k. pamoja na kutoa ushauri mbalimbali ili kuweza kuepukana na Saratani ambazo ni ugonjwa hatari sana, ambao hautambuliki kabisa na wananchi walio wengi.