KAMPUNI YA FASTHUB SOLUTION WAJITOKEZA KUFANYIWA UCHUCHUZI WA AWALI WA SARATANI YA MATITI KATIKA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD

      Comments Off on

KAMPUNI YA FASTHUB SOLUTION WAJITOKEZA KUFANYIWA UCHUCHUZI WA AWALI WA SARATANI YA MATITI KATIKA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD

Kampuni ya fasthub Solution inayojishughulisha na masuala mbalimbali ya mawasiliano ikiwamo utumaji wa msg za jumla kwa watu wengi (bulk msg) mapema leo wamefika katika Taasisi ya Saratani Ocean Road kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi wa awali, ushauri wa Magonjwa ya saratani pamoja na ushauri wa namna ya kujikinga na saratani hiyo.

Akizungumza wakati anawapa ushauri huo, Dr. Maguha Stephano amesema kuwa ugonjwa wa Saratani ni ugonjwa hatari sana ambapo kw kina mama husumbuliwa zaidi na matiti na mlango wa kizazi huku wanaume wakihangaika na saratani ya Tezi Dume.

Aidha Dkt Maguha amewasisitiza kuwa ugonjwa wa Saratani ni hatari lakini watu wengi hawajui kuhusu ugonjwa huu hivyo kuwaasa kuwa baada ya kupata vipimo hivi wanapoondoka wakawe mabalozi wazuri na kushirikiana kusambaza huduma hizo ili zikawasaidie wananchi wengine pindi wapatapo ujumbe kutoka kwao na kufika mara moja kwaajili ya uchunguzi.

Nao kwa upande wao wameoshukuru Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa kuwapa mapokezi mazuri na kupewa huduma ya kipekee ambapo wameahidi kuyafanyia kazi yale yote waliyofunzwa.

Taasisi hii imeitumia kampuni ya Fasthub kwa mwezi huu wa uelewa ywa Saratani ya matiti kutuma msg zaidi ya Laki moja, ili kuweza kuwasaidia watu mbalimbali kutambua kuhusu Saratani hii.

Taasisi ya Saratani Ocean Road huwa na utaratibu wa kufanya kazi ya utoaji na vipimo vya awali kwa wananchi pamoja na makampuni mbalimbali huku mashirika yale ya kiserikali na yale yasiyo ya kiserikali, lengo ni kusaidia watu kutambua ukweli juu ya ugonjwa huu hatari na kuufanyia kazi, hivyo watu wote wanakaribishwa kufika na kupata huduma hii ya uchunguzi.