MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD AKIZUNGUMZA NA WAGONJWA KUHUSU BIMA YA AFYA KWA WOTE NA NAMNA AMBAVYO ITAKAVYOWEZA KUWASAIDIA

      Comments Off on

MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD AKIZUNGUMZA NA WAGONJWA KUHUSU BIMA YA AFYA KWA WOTE NA NAMNA AMBAVYO ITAKAVYOWEZA KUWASAIDIA

Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. Julius Mwaiselage, asubuhi ya leo amewafikia wateja zaidi ya 340 katika maeneo mbalimbali ya kusubiria wagonjwa katika Taasisi hiyo alipokuwa akizungumza na wateja hao kuhusu Bima ya Afya kwa wote na namna ambavyo itakavyoweza kuwasaidia wananchi kwenye matibabu ya Saratani.

Dkt Mwaiselage amesema kuwa baadi ya Dawa za Saratani zinagharimu pesa nyingi sana ambazo katika hali ya kawaida baadhi ya wanachi hawawezi kuzimudu gharama hizo hivyo kujiunga na mfuko huu, kutasaidia kupunguza shida hizo kwa wananchi.

Akigusia suala la umuhimu wa Bima hiyo, Dkt mwaiselage amesema kuwa moja kati ya faidq kubwa sana ya bima hii ni kuwa, itawasaidia watu kupanga mipango yao ya kimaendeleo kwani kipindi ambacho ugonjwa umewapata hawatofikiria Tena kulipia pesa, Bali Bima hiyo itafanya kazi ya kulipia matibabu hayo.

Aidha ameipongeza serikali ya awamu ya Sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kupitia wizara ya Afya kwa kufikiria jambo km hili na kujali wananchi wake kwani wananchi wengi wamekuwa wakipoteza maisha na kuacha deni ambalo ni vigumu kwa familia kulilipa.

Katika hatua nyingine Dkt. Mwaisalage amesisitiza kuwa wananchi kuwa wavumilivu wakati serikali ikishughulikia jambo hili kupitishwa bungeni na kuwa sheria itakayowasaidia watanzania wengi sana

Nae bi Asia Salum amemshukuru Dr. Mwaiselage kwa kuwafahamisha kuhusu jambo hilo na kuiomba serikali kuharakisha mchakato huo kwani utakuwa ni kombozi kwa jamii nyingi za watanzania.