UJENZI ICU YA KISASA WAFIKIA 99%, MRI 100% HUDUMA ZA TIBA ZAZIDI KUMAILIKA KATIKA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD(ORCI)

      Comments Off on

UJENZI ICU YA KISASA WAFIKIA 99%, MRI 100% HUDUMA ZA TIBA ZAZIDI KUMAILIKA KATIKA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD(ORCI)

Bodi ya wadhamini katika Taasisi ya Saratani Ocean Road leo majira ya asubuhi wametembelea Miradi kadhaa inayotekelezwa kupitia fedha za IMF katika Taasisi hiyo.

Akizungumza wakati anatoa taarifa fupi kuhusu mradi wa ICU, mratibu wa Miradi ya IMF katika Taasisi hiyo ndg Mohammed Mbwana, amesema kuwa, mradi huo utakaochukua zaidi ya wagonjwa mahututi 24 umegharimu jumla ya kiasi cha shilingi milioni 800 mpaka kumalizika kwake.

Wakati huohuo Bw. Mbwana amesema kuwa mradi huu umetekelezwa kwa kufata taratibu zote za kimanunuzi na kwamba hakuna mwanya wowota uliotumika kupitish pesa kwa utaratibu au matumizi mengine tofauti na iliyokusufiwa.

Nae mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage amewaeleza wajumbe wa bodi kwamba thamani ya fedha imesimamiwa katika ujenzi na vifaa ambavyo vina mkataba matengenezo kinga ya miaka mitano

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi hiyo ya wadhamini Prof Ephata Kaaya amewapongeza uogozi wa Taasisi hiyo kwa kuweza kusimamia jengo hilo, ambapo litakuwa tayari kwaajili ya matumizi punde tu vifàa vingine vitakapomaliziwa kufungwa.