ZOEZI LA TATHIMINI YA KUKINGA NA KUTHIBITI MAAMBUKIZI YA MAGONJWA (IPC)

      Comments Off on

ZOEZI LA TATHIMINI YA KUKINGA NA KUTHIBITI MAAMBUKIZI YA MAGONJWA (IPC)

Kitengo Cha kuboresha huduma Cha Wizara ya Afya pamoja na Timu ya Taasisi ya Saratani Ocean Road ikiwa tayari kabisa kuanza zoezi la tathimini ya kukinga na kuthibiti maambukizi ya magonjwa (IPC), baada ya kupata baraka zote kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage.

Aidha Dkt. Mwaiselage ameitaka timu ya ORCI kuwa tayari kupokea tathimini hiyo kutoka kwa wakaguzi hao wa Wizara ya Afya, na kuweza kuifanyia kazi katika kuboreshq mapungufu yoyote yale ambayo yanaweza kujitokeza.

Kwa upande wa wakaguzi kutoka wizara ya Afya wanasema kuwa tathimini hiyo ya IPC itakuwa katika viwango vya Kimataifa, hivyo kuongeza ufanisi kwenye utendaji kazi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road huku lengo la tathimini ni kuona kama kuna mapungufu katika sehemu za kutolea huduma, kama zitakuwepo ili zifanyiwe kazi na kuendelea kuboresha katika maeneo yale yatakayokuwa yanafanya vizuri.

Zoezi hilo ambalo litakuwa ni maalum kwaajili ya mustakabali wa maendeleo ya Taasisi yetu, linakadiriwa kuchukua muda wa zaidi ya siku tano.