NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA DKT. SEIF SHEKALAGHE AMESEMA KUWA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD INATAKIWA IJIKITE KATIKA TAFITI ZA SARATANI PAMOJA NA KUTOA ELIMU YA UELEWA WA SARATANI KWA JAMII

      Comments Off on

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA DKT. SEIF SHEKALAGHE AMESEMA KUWA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD INATAKIWA IJIKITE KATIKA TAFITI ZA SARATANI PAMOJA NA KUTOA ELIMU YA UELEWA WA SARATANI KWA JAMII

Naibu katibu mkuu wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe amesema kuwa Taasisi ya Saratani Ocean Road inatakiwa ijikite katika Tafiti za Saratani pamoja na kutoa Elimu ya kutosha kwa jamii ili uwelewa uwe mkubwa jambo litakalopelekea kupungua kwa Maradhi ya Saratani.

Dkt. Shekalaghe ameyasema hayo mapema jana alipotembelea katika Taasisi hii ili kuweza kujionea namna huduma zinavyotolewa na pia kujionea mashine zinavyofanya kazi.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage amesema kuwa, wamepokea maelekezo hayo tayari kwa kuyafanyia kazi huku akisisitiza kuwa wataendelea kutoa huduma pamoja na kusimamia baadhi ya vituo vya Afya kama vile
Mtwara na Kigoma ambavyo kwasasa vipo chini ya Taasisi hii.

Akiendelea kwenye taarifa yake Dkt. Mwaiselage amesema kuwa Taasisi itajikita pia kwenye Tafiti za kibingwa pamoja na kuongeza Elimu kwa umma pamoja na kutoa Kinga kwa jamii ili kupunguza idadi ya watu watakaoathirika na ugonjwa huu huku wakiedelea kufanya ufatiliaji wa huduma zote za saratani zinazotolewa katika hospitali nyingine.