Taasisi ya Saratani Ocean Road imepeleka madaktari wake bingwa India huku lengo la safari hii ni kuwajengea uwezo madaktari na kuifanya Tanzania kuwa kituo cha Tiba utalii kwa nchi za Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Taasisi imewakilishwa na Dkt Caroline Swai, Daktari bingwa wa magonjwa ya Saratani, Dkt. Revelian Iramu Daktari bingwa wa radiolojia na Dkt. Bright Sangiwa Daktari bingwa wa mionzi Tiba kutika Taasisi ya Saratani Ocean Road.
Madaktari hawa wamepata fursa ya kutembelea Hospitali za Apollo, YASHODA, HCG, Sakra, BLK-Max, Fortis na Hospitali ya chuo kikuu cha Sharda na kujifunza mambo mengi ambayo watapata fursa ya kuja kuyatumia katika Taasisi hii.
Huu ni mpango madhubuti ulioasisiwa na serikali ili kuweza kuwapa ujuzi baadhi ya madaktari wa Hospitali na Taasisi zote za serikali ili waweze kuisaidia Tanzania katika sekta ya Afya nchini pamoja na walio nje ya Tanzania ambao huja kutibiwa nchini.