MWENYEKITI WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD DKT. JULIUS MWAISELAGE AMESEMA MAAZIMIO KARIBU YOTE YALIYOWEKWA KATIKA KIKAO KILICHOPITA CHA BARAZA YAMEKAMILIKA

      Comments Off on

MWENYEKITI WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD DKT. JULIUS MWAISELAGE AMESEMA MAAZIMIO KARIBU YOTE YALIYOWEKWA KATIKA KIKAO KILICHOPITA CHA BARAZA YAMEKAMILIKA

Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage amesema maazimio karibu yote yaliyowekwa katika kikao kilichopita Cha Baraza yamekamilika na kubaki maazimio machache ambayo yapo katika utekelezaji.

Hayo yamesemwa Katika kikao cha sita cha Baraza la Tano la wafanyakazi wa Taasisi ya Saratani Leo ndio ikiwa inakamilisha muda wake wa miaka mitatu.

Kikao hicho kimejadili Mambo mbalimbali ya Taasisi pamoja na mustakabali wa wafanyakazi wa Taasisi katika kuendeleza gurudumu la Maendeleo ya Taifa la Tanzania.

Dkt. Mwaiselage amesema kuwa Taasisi inaendelea kutoa huduma zote zinazotolewa katika Taasisi hiyo ikiwemo huduma za Kinga, huduma za uchunguzi, huduma za Tiba Mionzi na huduma nyinginezo.

Aidha Dkt. Mwaiselage amethibitisha kuwa Taasisi hiyo ipo salama isipokuwa kuna changamoto ndogo za kiubinadamu ambazo ameahidi kuzishughulikia na kuzimaliza kabisa.

Kutokana na Baraza hilo kufanya majukumu yake kwa muda wote wa miaka mitatu bila migogoro na kukubaliana Mambo yote ya Maendeleo katika Taasisi ya Saratani, kila mjumbe wa Baraza hilo ametunukiwa tuzo, ikiwa ni ishara ya kutambua mchango mkubwa wa kila mjumbe kwenye kujali maslahi ya wafanyakazi katika baraza hilo

Pamoja na hayo Dkt. Mwaiselage amewataka wajumbe watakaochaguliwa tena kwenye Baraza la Sita kumpa ushirikiano zaidi katibu atakayekuwepo katika Baraza lijalo.