WATUMISHI WA SHIRIKA LA UWAKALA WA MELI TANZANIA(TASAC) WAFANYIWA UCHUNGUZI WA SARATANI

      Comments Off on

WATUMISHI WA SHIRIKA LA UWAKALA WA MELI TANZANIA(TASAC) WAFANYIWA UCHUNGUZI WA SARATANI

Taasisi ya Saratani Ocean Road leo imeendeleza jukumu lake la kuwafanyia uchunguzi wa Saratani baadhi ya watumishi wa serikali ambapo safari hii watumishi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), wamefanyiwa uchunguzi mwishoni mwa wiki hii.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Bi. Beatrice Mushi, amesema, watumishi wa TASAC wametupa hamasa kubwa sana kwani wamejitokeza kwa wingi kuchunguzwa afya zao.

Taasisi ya Saratani imewafanyia uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa kizazi, Saratani ya Matiti, Saratani ya tezi dume pia na kuwafanyia kipimo Cha HIV pamoja na kipimo Cha Sukari.

Aidha Bi. Beatrice Mushi ametoa wito kwa Taasisi na mashirika mbalimbali ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali wajitokeze katika kufanya uchunguzi wa Afya zao ikiwemo uchunguzi wa maradhi ya Saratani sababu Saratani ikigundulika mapema inatibika.

“Natoa wito kwa mashirika mengine ya kiserikali na yale yasiyo ya kiserikali kuhakikisha kuwa wanafika katika Taasisi ya Saratani Ocean Road kufanya uchunguzi ili kuweza kupata matibabu mapema sababu Saratani ikigundulika mapema inatibika” Alimaliza Bi. Beatrice