TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD YASHINDA MASHINDANO MEI MOSI TAIFA 2024 YALIYOFANYIKA JIJINI ARUSHA

      Comments Off on

TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD YASHINDA MASHINDANO MEI MOSI TAIFA 2024 YALIYOFANYIKA JIJINI ARUSHA

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya saratani Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage amepokea vikombe vya ushindi vya Taasisi ya saratani Ocean Road katika mashimdano ya Mei Mosi Taifa 2024 yaliyofanyika mkoani Arusha.

Taasisi ya saratani Ocean Road imekuwa mshindi wa Kwanza katika mchezo wa bao kwa wanaume, huku ikishika nafasi ya tatu kwa wanaume kwenye mbio za baiskeli.

Dkt. Mwaiselage amewapongeza washiriki wote walio iwakilisha Taasisi katika mashindano hayo ya Mei Mosi huku akisema kuwa Taasisi ya Saratani ni kubwa na imebarikiwa kiasi kwamba pamoja na kutoa huduma za matibabu ya Saratani, wanashiriki na kushinda katika michezo mbalimbali.

Wakati huo huo Dkt. Mwaiselage kipekee amewapongeza mshindi wa Kwanza wa Bao Bw. Moshi Mteta na mshindi wa tatu wa mbio za Baiskeli Bw. Stephen Sanga, huku akisisitiza wengine kuongeza juhudi ili wakati ujao tupate makombe mengi zaidi.

Dkt. Mwaiselage amesisitiza ushiriki wa mazoezi kila jumamosi kama ishara ya kuunga mkono agizo la waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa lakini pia kujiweka katika hali ya kuepukana na athari za magonjwa yasiyoambukizwa.