KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA AFYA NA MASUALÀ YA UKIMWI IMETEMBELEA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD MAPEMA LEO 23/02/2024

      Comments Off on

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA AFYA NA MASUALÀ YA UKIMWI IMETEMBELEA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD MAPEMA LEO 23/02/2024

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI imetembelea Taasisi ya Saratani Ocean Road mapema leo tarehe 23/02/2024

ili kujionea utoaji wa huduma na miradi mbalimbali iliyopo katika Taasisi hiyo.

Kamati hiyo ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti, Mhe Dkt. Faustine Ndungulile wameipongeza Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa kuweza kuisimamia miradi inayotekelezwa kwa fedha nyingi kwa ustadi wa hali ya juu.

Miradi hiyo ikiwemo mradi mpya wa PET/CT Scan na Cyclotron ambao umeghalimu zaidi ya kiasi cha Shilingi bilioni 18, na upo tayari kwa kuanza kutumika mapema iwezekanavyo.

Miradi mingine ni wa mashine ya MRI, CT- Scan, na ujenzi wa jengo la Multipurpose Oncology.

Pamoja na hayo Dkt. Ndungulile ametoa pongezi kwa huduma bora na za kipekee zinazotolewa katika Taasisi hiyo ikiwemo misamaha ya takribani Tshs 2.2 bilioni kila mwezi hasa ukizingatia kuwa wengi wa watanzania hawana uwezo wa kujihudumia kutokana na maradhi hayo.

Aidha kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Mhe Dkt. Godwin Mollel amesema Serikali inaongeza jitihada za kupeleka huduma za saratani katika hospitali za kanda ili kuipunguzia mzigo Taasisi na tayari kanda zote zinahuduma ya tiba saratani; na kuongeza ya kwamba Wizara imeiagiza Ocean Road kujenga kituo cha saratani Mbeya na ujenzi utaanza katibuni. Aidha, amesema kwambw Wizara imepokea maelekezo na ushauri wa Kamati na itayafanyia kazi kwa ustawi wa sekta ya afya nchini.

Awali Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage akiwasilisha ripoti alieleza mafanikio mengi ya utoaji huduma za kinga, uchunguzi, tiba, mafunzo na utafiti pamoja na changamoto zilizopo katika Taasisi zinapungua kadiri muda unavyokwenda kwa kuwa serikali inatoa mchango mkubwa katika kukabiliana na changamoto hizo.