USIMIKAJI WA MASHINE YA PET/CT SCAN UMEFIKIA HATUA NZURI AMBAPO VIFAA VYOTE VYA MSINGI

      Comments Off on

USIMIKAJI WA MASHINE YA PET/CT SCAN UMEFIKIA HATUA NZURI AMBAPO VIFAA VYOTE VYA MSINGI

Usimikaji wa mashine ya PET/CT Scan umefikia hatua nzuri ambapo vifaa vyote vya msingi vimekamilika na kubakia kuunganisha mfumo wa umeme na vifaa vichache ili iweze kufanya kazi kama inavyotarajiwa.

Mashine hiyo ya PET/CT Scan ni utekelezaji wa maono ya Rais Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania katika kuboresha huduma za saratani nchini.

Mradi huu ulihusisha ujenzi wa jengo maalum la kusimika mashine za PET/CT Scan na Cyclotron, ambapo mpaka sasa mradi huo umegharimu kiasi cha Shilingi bilioni 18.2.

Mashine hiyo ambayo inatarajia kuanza kufanya kazi hivi karibuni, inauwezo mkubwa wa kugundua Saratani hata ikiwa katika hatua za awali kabisa.

Mashine hii pindi itakapokamilika, itasaidia kupunguza gharama kwa watanzania kwenda nje ya nchi huku ikitarajiwa kupokea wageni wengi zaidi kutoka nchi mbalimbali barani Afrika, kwani ni miongoni mwa mashine chache sana zenye uwezo mkubwa katika Bara hili.