Dc. Jokate ahimiza jamii kutembelea, kuwafariji wagonjwa

      Comments Off on

Dc. Jokate ahimiza jamii kutembelea, kuwafariji wagonjwa

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegero amepokea msaada wa vifaa tiba vilivyotolewa na Jema Foundation kwa ajili ya wagonjwa wanaopatiwa matibabu ya saratani katika Taasisi ya Saratani Ocean Road.

Taasisi hiyo inasimamiwa na Jema Baruani ambaye ni miongoni mwa wagonjwa waliowahi kutibiwa saratani Ocean Road na kupona sasa akijitolea kuendelea kuelimisha jamii kuhusu magonjwa hayo.

Akipokea msaada huo, amehimiza jamii kuendeleza utamaduni wa kuwatembelea, kuwajulia hali wagonjwa waliolazwa wodini, hospitalini walimolazwa ili kupatiwa matibabu dhidi ya maradhi mbalimbali yanayowakabili.

“Hakuna anayeijua kesho yake,” amesisitiza.

Dc jokate ametumia mfano hai wa shangazi yake ambaye alijiwekea utaratibu wa kuwatembelea na kuwasaidia wagonjwa pasipo kujua kwamba kitendo hicho siku moja kingekuwa msaada mkubwa kwake.

“Alikuwa anajitoa sana, kila alipotoka kazini aliwatembelea wagonjwa wa saratani, sasa hivi ni mstaafu, wakati alipokuwa anafanya vile hakuwahi kufikiri siku moja itakuwa sehemu muhimu ya kipenzi chake (mume wake), kwenda kutibiwa.

“Kwa hiyo, alipolazwa kwa matibabu, kwa kuwa yeye (shangazi) alikuwa tayari anafahamika, ilikuwa wepesi kusaidiwa pia. Tunayoyafanya sasa ni hazina ya maisha yetu ya baadae,” amesisitiza.

Amewapongeza Jema Foundation kwa kujitoa kwa jamii hususan wagonjwa wa saratani kwa kuwatembelea na kuwafariji kila mwaka.

“Nawapongeza madaktari na wataalamu wote wa Ocean Road kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuwahudumia wagonjwa hawa,” amesema.

Ameongeza “Kipekee naipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imesimika vifaa vya kisasa hapa Ocean Road na sasa tunashuhudia inapokea wagonjwa wengine pia kutoka nje ya Tanzania.

“Daktari (Crispin Kahesa), amenieleza kwamba wanapokea wagonjwa kutoka nje ya nchi kwa sababu kuna uwezekaji mkubwa umefanywa na Serikali kwa kusimika mashine ambazo wenzetu kwenye nchi zao hawana.

“Amenieleza, huduma za tiba ya saratani zinayopatikana Tanzania ni bora za viwango vya kimataifa na gharama ni nafuu kulinganisha na mataifa mengine.

“Haya ni mambo ambayo lazima tuwaambie Watanzania, wajue kwamba tuna vitu ambavyo wengine wanatamani kuwa navyo, waje wapatiwe huduma bora,” ametoa rai Mkuu huyo wa Wilaya.

Mwakilishi wa Jema Foundation, Jema Baruani amesema wagonjwa wengi wa saratani huwa na hofu pale wanapogundulika, wapo wengine ambao huacha matibabu.

“Si wote huwa na moyo wa ujasiri kama mimi, wapo wanaokata tamaa,  si wote wana uwezo wa kulikabili gonjwa hili, inabidi sisi ambao Mungu ametujalia, tujitoe katika hali na mali, kuwaona… unaweza ukaja hapa japo kuwaambia neno pole, ikawa ahueni kwao,” amesema.

Jema ametoa rai pia kwa jamii hususan vijana kuwa na ujasiri na kujitokeza kufanyiwa uchunguzi wa saratani kwani ikiwa kugundulika, mtu hupona baada ya matibabu.

Mkurugenzi wa Kinga wa ORCI na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani, Crispin Kahesa amesema kila mwaka inakadiriwa Tanzania kuna wagonjwa wa saratani zaidi ya 42,060 asilimia 13 ndiyo hufika hospitali ni takriban wagonjwa 12,600.

“Hawa wanaokuja hospitalini asilimia 70 ndiyo huweza kukaa na kuendelea na tiba, asilimia 30 huwa wanakatiza au wanapotea kwa sababu tofauti tofauti ikiwamo mtazamo na hofu waliyonayo juu ya ugonjwa huo.

“Lakini pia kwa sababu huduma hizi zipo mijini zaidi, inawezekana wanapotea kwa kuwa wana majukumu mengi, watu wana changamoto nyingi za kiuchumi na kijamii,” amebainisha.

https://matukionamaisha.blogspot.com/

Makabidhiano ya mashine mpya ya X-ray(digital x-ray machine) chini ya mpango wa MES(Managed Equipment System)

      Comments Off on

Makabidhiano ya mashine mpya ya X-ray(digital x-ray machine) chini ya mpango wa MES(Managed Equipment System)

Mashine hii inauwezo wa kuingiza vipimo vyote vya x-ray hivyo kusaidia kurahisisha huduma kwa wagonjwa na huondoa usumbufu wa kusubili vipimo kwa wagonjwa, pia itaongeza ufanisi na ubora wa vipimo kwani ni ya kisasa na inatumia huduma za kisasa.Pia machine hizi zimekuja na  vifaa vya kujulinda dhidi ya mionzi kwa watumiaji wa machine pamoja na wagonjwa

Mkurugenzi pamoja na Mkurugenzi wa Tiba na wafanyakazi wa Taasisi ya saratani ya ocean Road, Pamoja na wataalamu wa mionzi(x-ray) wakiwa katika picha ya pamoja katika makabidhiano ya mashine ya X-rays chini ya mpango wa MES(Managed Equipment System)

Mkurugenzi pamoja na Mkurugenzi wa Tiba na wafanyakazi wa Taasisi ya saratani ya ocean Road katika makabidhiano ya mashine ya X-rays chini ya mpango wa MES(Managed Equipment System)

Mkurugenzi pamoja na Mkurugenzi wa Tiba na wafanyakazi wa Taasisi ya saratani ya ocean Road wakikagua vifaa(protective gown) vya kujilinda dhidi ya mionzi
Mkurugenzi pamoja na Mkurugenzi wa Tiba na wafanyakazi wa Taasisi ya saratani ya ocean Road wakionyesha stika na mtaalam wa mashine za X-ray

Mkurugenzi pamoja na Mkurugenzi wa Tiba(kushoto, akiwa amevaa nguo ya kujikinga na mionzi) na wafanyakazi wa Taasisi ya saratani ya ocean Road wakisikiliza maelekezo kutoka kwa mtalaam wa mionzi

Mkurugenzi(kulia) wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road akitoa shukrani na kuwapongeza wa Taaalamu wa mionzi(x-ray) na wafanyakazi wote wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road walioshiriki katika makabidhiano hayo ya mashine chi ya mapango wa MES

Kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road

      Comments Off on Kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road

Kikao cha kwanza cha baraza la tano la wafanyakazi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road kilifanyika tarehe 27/08/2020 katika ukumbi wa mikutano wa Kibaha Conference Centre. Kikao hicho kilichohudhuriwa na wajumbe wa TUGHE taifa na mkoa kilianza saa tatu kamili asubuhi kwa sala maalumu ya kuliombea baraza, Taasisi na Taifa katika utekelezaji ulio bora wa majukumu.

Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja

Baada ya wajumbe kujitambulisha, Mwenyekiti Ndugu. Julius Mwaiselage, aliwashukuru wajumbe kwa kuhudhuria mkutano katika muda uliopangwa na kuelezea mafanikio ya kiujumla ambayo baraza iliyapendekeza katika vikao vilivyopita na Taasisi kuyatekeleza. Miongoni mwa mafanikio hayo ni:

    Katika kikao hicho, baraza lilisikiliza na kujadili:

      Wajumbe wa baraza wakisikiliza kwa umakini uwasilishwaji wa ripoti za baraza la wafanyakazi
Wajumbe wa baraza wakisikiliza kwa umakini uwasilishwaji wa ripoti za baraza la wafanyakazi
Wajumbe wa baraza wakisikiliza kwa umakini uwasilishwaji wa ripoti za baraza la wafanyakazi
Wajumbe wa baraza wakisikiliza kwa umakini uwasilishwaji wa ripoti za baraza la wafanyakazi