MGANGA MKUU WA MANISPAA YA  MPANDA DR. PAUL SWAKALA AMEISHUKURU TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD KWA KUWEZA KUFANYA MAAMUZI YA KUFIKA NA KUWAHUDUMIA KWA VIPIMO WANANCHI NA WAKAAZI WA MANISPAA HIYO.

      Comments Off on

MGANGA MKUU WA MANISPAA YA  MPANDA DR. PAUL SWAKALA AMEISHUKURU TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD KWA KUWEZA KUFANYA MAAMUZI YA KUFIKA NA KUWAHUDUMIA KWA VIPIMO WANANCHI NA WAKAAZI WA MANISPAA HIYO.

Mganga mkuu wa manispaa ya mpanda Dr. Paul Swakala ameishukuru Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa kuweza kufanya maamuzi ya kufika na kuwahudumia kwa vipimo wananchi na wakaazi wa manispaa hiyo.

Akizungumza na wakazi hao waliojitokeza kwa wingi kupima katika viwanja vya Kashato, Dr. Swakala amesema kuwa hivi ni vipimo muhimu sana hasa ukizingatia kuwa Taasisi ya Saratani Ocean Road wamekuja kuwafata wananchi ili waweze kupata huduma hiyo karibu kabisa ili kuwaepushia gharama za kufata huduma hizo Dar es Salaam.

Akiwakumbusha zaidi Dr. Swakala amesema kuwa madaktari waliokuja hapa nimabingwa kabisa hivyo amewataka wanampanda kujitokeza kwa wingi sana ili kuepusha kuwavunja moyo kwani wanahitaji wakati mwingine wafike hapa Mpanda.

Nae mkuu wa msafara wa Madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road na Meneja wa huduma za kinga wa Taasisi hiyo Dr. Maguha Stephano amewashukuru kina baba kwa kujitokeza kwa wingi mno zaidi ya kina mama ili kuweza kupata huduma ya vipimo vya Saratani ya Tezi Dume.

Aidha ameendelea kusisitiza kuwa wananchi wajitokeze zaidi kwani wapo katika kampeni hiyo kwa siku Tatu kuanzia tarehe 18 mpaka 20 Julai ili kuweza kuwasaidia wananchi wengi zaidi huku akisema kuwa huduma zote zitatolewa bure kabisa

“Nasisitiza wananchi kujitokeza kupata vipimo kwa wingi kwani tupo kwenye kampeni hii kwa muda wa siku tatu kuanzia leo jumatatu Tarehe 18 mpaka tarehe 20 mwezi huu, na huduma hii inatolewa bure kabisa hivyo karibuni sana.” Alimaliza Dr. Maguha.

Timu ya Madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, ipo mkoa wa Katavi katika Manispaa ya Mpanda ili kuweza kutoa huduma za upimaji wa aina mbalimbali za Saratani na magonjwa mengine km kisukari, presha n.k. pamoja na kutoa ushauri mbalimbali ili kuweza kuepukana na Saratani ambazo ni ugonjwa hatari sana, ambao hautambuliki kabisa na wananchi walio wengi.

HONGERENI KWA KUTOA CHANJO YA UVIKO-19 ILA ONGEZENI HAMASA- WAZIRI UMMY MWALIMU

      Comments Off on

HONGERENI KWA KUTOA CHANJO YA UVIKO-19 ILA ONGEZENI HAMASA- WAZIRI UMMY MWALIMU

Waziri wa Afya Mh. Ummy mwalimu ameipongeza Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa kuamua kuhamasisha watu kupata chanjo ya UVIKO-19 

Akizungumza ndani ya viwanja vya maonesho ya kimataifa ya kibiashara alipotembelea  katika banda la Taasisi ya Saratani Ocean Road waziri Mwalimu amesema kuwa Taasisi hiyo imejitahidi sana kwenye utoaji wa chanjo hiyo huku akisema kuwa idadi iliyotajwa kwa watu waliopewa chanjo hiyo bado ni ndogo hivyo kuwaasa waongeze nguvu ili kuweza kupata idadi kubwa zaidi.

Awali akitoa wasilisho la Taasisi Afisa mawasiliano na uhusiano wa Taasisi hiyo Bw. Islam Mposso amesema kuwa mpaka muda ambao Mh. Mwalimu anapita tayar watu zaidi ya 34 walikwishapatiwa chanjo ya UVIKO-19.

Taasisi ya Saratani Ocean Road inashiriki maonesho ya 46 ya kimataifa ya biashara ambapo inatoa huduma za upimaji ws saratani ya Tezi Dume, Matiti, Ngozi ka watu wenye Ualbino, Mlango wa kizazi kwa wakina mama, hata hivyo inatoa pia huduma ya upimaji na utoaji chanjo ya homa ya Ini pamoja na UVIKO-19

TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD YAENDELEA NA HUDUMA KATIKA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA KIBIASHARA(SABASABA)

      Comments Off on

TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD YAENDELEA NA HUDUMA KATIKA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA KIBIASHARA(SABASABA)

Taasisi ya Saratani Ocean Road imeendelea na utoaji wa huduma za uchunguzi wa awali kwa Saratani ya Mlango wa Kizazi, Tezi Dume, Saratani ya Matiti na ile ya ngozi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) katika mabanda yao yaliyopo ndani ya viwanja vya maonesho ya biashara ya kimataifa vya Sabasaba.Akizungumzia kuhusu

Uchunguzi huo kaimu mkurugenzi wa kinga Dr. Maguha Stephano amesema kuwa uchunguzi huo unafanyika bila malipo yoyote yale, hivyo amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kupima Afya zao.

Aidha Dr. Stephano amesema kuwa pamoja na uchunguzi huo pia wanatoa huduma ya upimaji wa homa ya Ini pamoja chanjo yake, pia huduma ya chanjo ya UVIKO-19 ipo.

Dr. Stephano amesisitiza wananchi kutembelea banda hilo na kupata elimu kuhusu ugonjwa wa Saratani kwani ugonjwa huu ni hatari kuliko baadhi ya magonjwa yanayodhaniwa ni hatari ila kwakuwa bado elimu haijawafikia wanaudharau.

“Naendelea kusisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika banda letu ili kuweza kupata elimu sahihi ya ugonjwa huu, kwani ugonjwa huu ni hatari sana ukilinganisha  na baadhi ya magonjwa ambayo hudhaniwa hatari na kuudharau ugonjwa huu kutokana na kukosa elimu juu ya uhatari wake”. Alisema Dr. Stephano.

WAZIRI WA AFYA MH. UMMY MWALIMU AMEZINDUA RASMI BODI MPYA YA UDHAMINI KATIKA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROADi

      Comments Off on

WAZIRI WA AFYA MH. UMMY MWALIMU AMEZINDUA RASMI BODI MPYA YA UDHAMINI KATIKA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROADi

Mapema leo Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu amezindua Rasmi Bodi mpya ya udhamini katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo katika Taasisi ya Saratani Ocean Road.


Akizungumza katika uzinduzi huo Mheshimiwa Mwalimu amesema kuwa kati ya Taasisi zaidi ya 40 zilizo chini ya wizara ya Afya, Taasisi ya Saratani Ocean Road ipo katika Tatu bora kwa kutokuwa na makandokando ya lawama kutoka kwa Wananchi.
Aidha Waziri mwalimu ameushukuru uongozi wa bodi iliyoisha muda wake na kusema kuwa waliingia katika kipindi kigumu sana lakini waliweza kupambana kwa kuweka mipango sawa mpaka Taasisi kufikia hapa ilipo sasa.
Nae mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dr. Julius Mwaiselage amepongeza jitihada zilizofanywa na uongozi uliopita ambao ulikuwa chini ya profesa Hamisi Dihenga kwa kuifikisha Taasisi hapa ilipo.


Profesa Dihenga amemaliza muda wake na kuteuliwa kuwa Mwenekiti wa bodi ya bodi ya mikopo nchini Tanzania na kumpisha Profesa Kaaya na timu yake ya watu nane kuiongoza bodi hiyo ili kusukuma gurudumu la utoaji huduma mbele

Mganga Mkuu wa Serikari aongoza Mashujaa wa Saratani

      Comments Off on

Mganga Mkuu wa Serikari aongoza Mashujaa wa Saratani

Mganga mkuu wa Serikari Dr Aifello Sichwale mapema mwishoni mwa wiki hii ameongoza mamia ya wadau na wahanga mbalimbali katika matembezi ya hisani ya kuhimiza watanzania na watu wote kupima mapema Saratani na kupata matibabu ili kuepuka madhara zaidi ya kuchelewa kupata huduma.

Akizungumza katika maadhimisho ya matembezi hayo yaliyoanzia katika Taasisi ya Saratani Ocean Road Dr Sichwale amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa kupima Saratani kwani inapogundulika mapema inakusaidia kupata matibabu ya haraka na kuepukana na vifo visivyotarajiwa, hivyo amewataka watanzania kufanya hivyo mapema sana ili kupata nafuu hiyo.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dr. Mwaiselage amesema kuwa wanaishukuru sana Serikali kwa kuweza kufanikisha upatikanaji wa Dawa ambapo wananchi wengi wamekuwa wakipata tiba sahihi inayostahili.

Aidha Dr. Mwaiselage amewaasa watanzania kutoogopa kuja kupima kwa kuhofia kipato kwani upimaji huu ni bure na pia kwa upande wa Matibabu wamekuwa wakiwasaidia wananchi kulipa baadhi ya Matibabu hayo kupitia kitengo cha Ustawi wa Jamii ambapo Wananchi hufika hapo na kusaidiwa baadhi ya gharama hizo.

Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka ili kuweza kutoa msisitizo kwa wananchi kuweza kupata vipimo mapema ili kujua Afya zao na km itatokea wamegundulika na Saratani waweze kupata matibabu ili kuepuka madhara makubwa ambayo mwisho wa siku hupelekea vifo.

Kipimo cha damu chaibua wanaume 8% viashiria saratani tezidume – Njombe

      Comments Off on

Kipimo cha damu chaibua wanaume 8% viashiria saratani tezidume – Njombe

Wanaume tisa sawa na asilimia 8 ya wanaume 103 waliojitokeza kwenye kampeni maalum ya uchunguzi wa awali kwa magonjwa ya saratani, wamekutwa na saratani ya tezidume, Mkoani Njombe.

Kampeni hiyo imefanywa na wataalamu mabingwa wa Taasisi ya Saratani Ocean Road {ORCI} ndani ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe kwa siku tatu {April 8 hadi 10} kwa ufadhili wa benki ya NBC., Akizungumza Meneja Kitengo cha Uchunguzi wa Saratani {ORCI}, Dkt. Maguha Stephano amesema wanaume hao walichunguzwa kwa kipimo cha damu {PSA} na kwamba wamepewa rufaa kufika Ocean Road kwa matibabu zaidi.

Amebainisha kwamba kiujumla watu 600 waume kwa wake walijitokeza kwenye kampeni hiyo kufanya uchunguzi wa afya zao. “Wanawake 497 walijitokeza ni sawa na asilimia 83 ya wote waliofika kwa ajili ya uchunguzi wa afya zao na 103 sawa na asilimia 17 ni wanaume,” amefafanua. Amesema wanawake saba walikuwa na uvimbe kwenye matiti, wawili walikutwa na viashiria vya awali vya saratani ya matiti.

“Wanawake wengine walichunguzwa saratani ya mlango wa kizazi, 10 walikutwa na mabadiliko ya awali (precancerous lesions) na walipatiwa tiba (cryotherapy) ili kuzuia saratani ya mlango wa kizazi. Amesema wanawake wawili walikutwa na saratani ya mlango wa kizazi na kupewa rufaa kwenda Ocean Road.

Wananchi wajitokeza kampeni ya saratani Njombe

      Comments Off on

Wananchi wajitokeza kampeni ya saratani Njombe

Wanaume tisa wakutwa na viashiria vya Saratani ya tezi dume ambao ni sawa na Asilimia 17 ya waliojitokeza kwenye kampeni ya uchunguzi wa saratani ya tezi dume mkoani Njombe.
Hayo yamebainishwa na Meneja Kitengo cha Uchunguzi wa Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt. Maguha Stephano kwenye  kampeni ya uchunguzi wa Saratani iliofanyika mkoani Njombe na kuhudhuriwa na wananchi 600 huku wengi wao wakiwa ni akina mama. 
Amesema Wanaume walijitokeza walikua 103 sawa na asilimia 17, waliopimwa na kukutwa na viashiria hivyo vya Saratani ya tezi dume na walipewa rufaa ya kwenda taasisi ya Saratani ocean road kwa uchunguzi zaid na matibabu.


Kwa upande wa Wanawake Dkt. Maguha amesema Wanawake waliojitokeza ni 497 sawa na asilimia 83 huku wanaume wakiwa 103 sawa na asilimia 17 na kufanyiwa vipimo vya magonjwa mbalimbali ya Saratani. 
“Wanawake Saba ambao walifanyiwa uchunguzi wa Saratani ya matiti walikutwa na uvimbe na wawili walikuwa na viashiria vya Saratani ya matiti”.
Pia, wanawake wengine waliofanyiwa uchunguzi wa Saratani ya mlango wa kizazi 10 walikutwa na mabadiliko ya awali ya Saratani ya mlango wa kizazi (precancerous lesions) na walipatiwa tiba (cryotherapy) ili kuzuia saratani ya mlango wa kizazi na wanawake wawili walikutwa na Saratani ya mlango wa kizazi na kupewa rufaa kwenda Ocean road.
Kampeni hiyo ya uchunguzi wa Saratani mkoani Njombe ilianza tarehe 8 mpaka 10 April, 2022 na kutolewa kwa wananchi wote bila malipo.

Nilipokutwa na saratani ya titi, ‘nilikata tamaa ya maisha, ila miaka kumi baadae…’ – Lucy

      Comments Off on

Nilipokutwa na saratani ya titi, ‘nilikata tamaa ya maisha, ila miaka kumi baadae…’ – Lucy

Bwana: Majibu ya maabara kwamba amekutwa na saratani ya matiti iliyofikia hatua ya tatu, miaka 11 iliyopita haikuwa rahisi kwa Lucy kuyapokea.
Daktari wake alipomjulisha juu ya majibu hayo, fikira zake ‘zilimsafirisha’ hadi kuanza kutafakari namna mazishi na maziko yake yatakavyokuwa.
Akisimulia mbele ya mashujaa zaidi ya 30 wa saratani {Waliotibiwa na kupona na wanaoendelea na matibabu dhidi ya maradhi hayo}, Taasisi ya Saratani Ocean Road, Lucy amesema alifanyiwa upasuaji na kuondolewa titi lake ili kuokoa maisha. 


Mashujaa hao wamekutanishwa leo katika ukumbi wa Nyerere ndani ya taasisi hiyo na Chama cha Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani {TOS} kupewa semina maalum iliyolenga kuwapa uelewa jinsi ya kuishi na kukabiliana na changamoto baada ya kukutwa na magonjwa hayo. 
Lucy amesema wagonjwa wa saratani hukumbana na mikasa mingi na ikiwa mtu hana taarifa sahihi wapo ambao huacha matibabu na kukimbilia kwengineko.
Akiendeleza simulizi yake ilivyokuwa  siku hiyo alipopewa majibu, amesema alitafakari pia namna gani ataweza kumudu ukurasa mpya wa maisha atakayoishi, akiwa na saratani.
“Ilikuwa 2010, mume alikuwa ameshafariki 2006, Hivyo nilitafakari juu ya watoto wangu waliokuwa na mdogo wakati huo, watabakije bila mama, wala baba.
“Ilinipa wakati mgumu, kiasi cha kushindwa kurejea nyumbani mwenyewe, ilibidi ndugu zangu wanifuate siku hiyo,” amesimulia.


Amesema alijawa na msongo wa mawazo na hilo lilichangiwa na uelewa duni aliokuwa nao kipindi hiçho kuhusu ugonjwa wa saratani.
“Nilikuwa sijui satatani ni nini, nilichokuwa nafahamu, mtu akiugua anakufa, nilijua ni ugonjwa wa watu wengine si wangu yaani sitakaa itokee niambiwe nina saratani.
“Lakini nikakutwa nayo, ilianza uvimbe mdogo na niliouna siku moja nilipoamka asubuhi, sikuwa na maumivu yoyote awali, niliendelea na shughuli zangu,” amesimulia.
Lucy amesema uvimbe uliendelea kukua na maumivu yalianza kubisha hodi, alilazimika kwenda hospitali hatimaye akagundulika kuwa na saratani hiyo.[28/10, 07:56] Bwana: Lucy amewasisitiza mashujaa wenzake wasiogope, wasisikilize taarifa potofu kuhusu saratani na wasiache matibabu kwani inatibika na mtu anapona kabisa kama ilivyokuwa kwake.
“Nimepona na nimezidi kuwa mrembo baada ya matibabu, nimeolewa na wanangu wamekuwa wakubwa maisha yanaendelea kama kawaida,” amesema
Mariam Isaya amesema semina hiyo imemsaidia kujifunza mengi na kumpa ujasiri zaidi kuendelea kupambana dhidi ya saratani ya kizazi aliyokutwa nayo.
Naye, Juma Kassim ameshukuru uongozi wa chama hicho kuandaa semina hiyo, kwani amekutana na mashujaa wenzake imempa imani kwamba hayupo peke yake na ipo siku atapona na kuwa historia.[28/10, 07:57] Bwana:

Akizungumza kwa niaba ya Rais wa TOS, Katibu wa Chama hiyo, Dk. Caroline Swai  {pichani} amesema semina hiyo imeandaliwa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yao kuhakikisha jamii inapata uelewa wa kutosha juu ya saratani mbalimbali.
Amesema wagonjwa wa saratani wanakutana na mabadiliko kadhaa kipindi cha matibabu, hivyo ni muhimu kuzidi kuwapa elimu sahihi jinsi gani wataweza kukabiliana nayo.
Amesema elimu inatolewa kwa mbinu mbalimbali pia ikiwamo kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.


Dk. Jennifer amesema Chama hicho ni kipya kimezinduliwa Novemba, mwaka jana na kwamba kimedhamiria kuifikia jamii hadi vijijini, kuielimisha.[28/10, 07:57] Bwana: Tuna jukumu kuu la kuhakikisha pia zile huduma wanazopewa wagonjwa zinakidhi viwango sawa na vile vinavyofanyika mataifa yaliyoendelea.
“Akitibiwa hapa akienda Marekani akute huduma ni Ile ile, tunayotoa hapa Tanzania. Apate huduma bora, tumejikita nyanja mbalimbali kuhakikisha huduma zinakuwa bora, tunafanya tafiti pia,” amebainisha.