KAMPUNI YA FASTHUB SOLUTION WAJITOKEZA KUFANYIWA UCHUCHUZI WA AWALI WA SARATANI YA MATITI KATIKA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD

      Comments Off on

KAMPUNI YA FASTHUB SOLUTION WAJITOKEZA KUFANYIWA UCHUCHUZI WA AWALI WA SARATANI YA MATITI KATIKA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD

Kampuni ya fasthub Solution inayojishughulisha na masuala mbalimbali ya mawasiliano ikiwamo utumaji wa msg za jumla kwa watu wengi (bulk msg) mapema leo wamefika katika Taasisi ya Saratani Ocean Road kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi wa awali, ushauri wa Magonjwa ya saratani pamoja na ushauri wa namna ya kujikinga na saratani hiyo.

Akizungumza wakati anawapa ushauri huo, Dr. Maguha Stephano amesema kuwa ugonjwa wa Saratani ni ugonjwa hatari sana ambapo kw kina mama husumbuliwa zaidi na matiti na mlango wa kizazi huku wanaume wakihangaika na saratani ya Tezi Dume.

Aidha Dkt Maguha amewasisitiza kuwa ugonjwa wa Saratani ni hatari lakini watu wengi hawajui kuhusu ugonjwa huu hivyo kuwaasa kuwa baada ya kupata vipimo hivi wanapoondoka wakawe mabalozi wazuri na kushirikiana kusambaza huduma hizo ili zikawasaidie wananchi wengine pindi wapatapo ujumbe kutoka kwao na kufika mara moja kwaajili ya uchunguzi.

Nao kwa upande wao wameoshukuru Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa kuwapa mapokezi mazuri na kupewa huduma ya kipekee ambapo wameahidi kuyafanyia kazi yale yote waliyofunzwa.

Taasisi hii imeitumia kampuni ya Fasthub kwa mwezi huu wa uelewa ywa Saratani ya matiti kutuma msg zaidi ya Laki moja, ili kuweza kuwasaidia watu mbalimbali kutambua kuhusu Saratani hii.

Taasisi ya Saratani Ocean Road huwa na utaratibu wa kufanya kazi ya utoaji na vipimo vya awali kwa wananchi pamoja na makampuni mbalimbali huku mashirika yale ya kiserikali na yale yasiyo ya kiserikali, lengo ni kusaidia watu kutambua ukweli juu ya ugonjwa huu hatari na kuufanyia kazi, hivyo watu wote wanakaribishwa kufika na kupata huduma hii ya uchunguzi.

MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD AKIZUNGUMZA NA WAGONJWA KUHUSU BIMA YA AFYA KWA WOTE NA NAMNA AMBAVYO ITAKAVYOWEZA KUWASAIDIA

      Comments Off on

MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD AKIZUNGUMZA NA WAGONJWA KUHUSU BIMA YA AFYA KWA WOTE NA NAMNA AMBAVYO ITAKAVYOWEZA KUWASAIDIA

Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. Julius Mwaiselage, asubuhi ya leo amewafikia wateja zaidi ya 340 katika maeneo mbalimbali ya kusubiria wagonjwa katika Taasisi hiyo alipokuwa akizungumza na wateja hao kuhusu Bima ya Afya kwa wote na namna ambavyo itakavyoweza kuwasaidia wananchi kwenye matibabu ya Saratani.

Dkt Mwaiselage amesema kuwa baadi ya Dawa za Saratani zinagharimu pesa nyingi sana ambazo katika hali ya kawaida baadhi ya wanachi hawawezi kuzimudu gharama hizo hivyo kujiunga na mfuko huu, kutasaidia kupunguza shida hizo kwa wananchi.

Akigusia suala la umuhimu wa Bima hiyo, Dkt mwaiselage amesema kuwa moja kati ya faidq kubwa sana ya bima hii ni kuwa, itawasaidia watu kupanga mipango yao ya kimaendeleo kwani kipindi ambacho ugonjwa umewapata hawatofikiria Tena kulipia pesa, Bali Bima hiyo itafanya kazi ya kulipia matibabu hayo.

Aidha ameipongeza serikali ya awamu ya Sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kupitia wizara ya Afya kwa kufikiria jambo km hili na kujali wananchi wake kwani wananchi wengi wamekuwa wakipoteza maisha na kuacha deni ambalo ni vigumu kwa familia kulilipa.

Katika hatua nyingine Dkt. Mwaisalage amesisitiza kuwa wananchi kuwa wavumilivu wakati serikali ikishughulikia jambo hili kupitishwa bungeni na kuwa sheria itakayowasaidia watanzania wengi sana

Nae bi Asia Salum amemshukuru Dr. Mwaiselage kwa kuwafahamisha kuhusu jambo hilo na kuiomba serikali kuharakisha mchakato huo kwani utakuwa ni kombozi kwa jamii nyingi za watanzania.

54 WAKUTWA NA VIASHIRIA VYA SARATANI ARUSHA.

      Comments Off on

54 WAKUTWA NA VIASHIRIA VYA SARATANI ARUSHA.

Idadi ya watu 54 wamekutwa na viashiria vya Saratani mbalimbali katika kampeni ya uchunguzi wa awali wa Saratani jijini Arusha.

Akizungumza katika kampeni hiyo, Meneja kitengo cha uchunguzi wa Saratani, Dkt Maguha Stephano amesema kuwa idadi hiyo imetokana na uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa kizazi kwa wateja 221 huku wale waliojitokeza kwaajili ya Saratani ya matiti wakiwa ni 257 na wale wa Tezi dume ni 362.Katika hatua nyingine Dr. Maguha amewahimiza wananchi wa eneo Hilo na maeneo mengine kwa ujumla kuhakikisha kuwa wànakuw na mtindo bora wa maisha ikiwa ni pamoja na kula matunda kwa wingi katika milo Yao yote.

Vile vile amewaasa kupunguza vyakula vyenye mafuta huku akiwasisitizia kufanya mazoezi mara kwa mara huku wakitakiwa kutumia vilevi kwa kiasi kidogo kama sio kuacha ili kuepukanaa na athari za magonjwa ya saratani.Kampeni hii imedumu kwa muda wa siku nne kuanzia tarehe 24 – 27 ya mwezi huu wa tisa

TUTASHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZOTE ZA SARATANI – MH. UMMY MWALIMU

      Comments Off on

TUTASHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZOTE ZA SARATANI – MH. UMMY MWALIMU

Mh. Ummy Mwalimu ameahidi kushighulikia changamoto zozote zitakazojitokeza za Saratani katika nchi ya Tanzania ikiwamo na uwekaji wa mikaka madhubuti ili kuweza kuudhi its ugonjwa huo.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi taarifa ya kiuchunguzi iliyofanywa na Lancet Oncology katika ukumbi wa mikutano kwenye hoteli ya Hyatt Regency, mapema mwanzoni mwa wiki hii, waziri mwalimu amesema kuwa kiwango cha watu wanaopoteza maisha kutokana na Saratani ni kikubwa mno ukilinganisha na kile cha UVICO-19, kwani kwa mwaka 2020 pekee watu zaidi ya 25,000 wamepoteza maisha, huku ikikadiriwa kuwa idadi hiyo kuongezeka hadi kufikia watu 1,000,000 kw mwaka ifikapo 2030.

Waziri Mwalimu a.esema kuwa kutokan na takwimu hizo, serikali itaweka mikakati mahususi kuhakikisha tatizo hilo linatowekaKatika hatua nyingine, waziri mwalimu amesema kuwa serikali ipo katika mpango wa kutudisha tena chanjo kwaajili ya wasichana wa kua zia umri wa miaka 9-14 kujikinga na Saratani ya Mlango wa Kizazi.Akizungumzia zaidi jambo hilo, waziri mwalimu ametanabaisha kuwa chanjo hiyo ni kweli imeonekana kusua sua kutokana na baadhi ya watu kusema kuwa chanjo hiyo ina madhara makubwa ikiwamo kutopata ujauzito na matatizo mengine ya Afya ya uzazi hali ambayo sio kweli, kwani serikali imefanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa chanjo hizo ni salama kabisa hivyo wataendelea kutoa chanjo hizo ili kunusuru maisha ya watoto hao kutokana na Saratani

RIPOTI YA ZOEZI LA UCHUNGUZI WA SARATANI MKOANI ARUSHA 24 – 26 SEPT 2022.

      Comments Off on

RIPOTI YA ZOEZI LA UCHUNGUZI WA SARATANI MKOANI ARUSHA 24 – 26 SEPT 2022.

Uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi jumla ya wanawake 221
Waliokutwa na mabadiliko ya awali na kupewa tiba. 16
Waliokutwa na viashiria vya saratani na kuchukuliwa vipimo kwa uchunguzi zaidi katika Taasisi ya Saratani Ocean Road ni 6
Saratani ya matiti jumla ni 247
Waliokutwa na vivimbe 8
Wamepewa rufaa kwa uchunguzi zaidi

Saratani ya tezi dume jumla ni 362
Waliokuwa na kiwango kikubwa cha PSA / kiashiria 24

Nawahimiza wananchi kuwa na mtindo bora wa maisha, ikiwa ni pamoja na kula mbogamboga na matunda kwa wingi katika milo yao,kupungua vyakula vyenye mafuta na sukari kwa wingi, kufanya mazoezi mara kwa mara, kuepuka matumizi ya tumbaku na kuepuka unywaji wa pombe kupita kiasi Kuwa na tabia ya kucheki afya zao mara kwa mara hata kama hawajisikii kuwa na dalili za ugonjwa wowote

MAPEMA LEO TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD KWA KUSHIRIKIANA NA CHAMA CHA MADAKTARI TANZANIA, WAMEFANYA UCHUNGUZI WA SARATANI MBALI MBALI KATIKA VIWANJA VYA AZIMIO MJINI ARUSHA

      Comments Off on

MAPEMA LEO TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD KWA KUSHIRIKIANA NA CHAMA CHA MADAKTARI TANZANIA, WAMEFANYA UCHUNGUZI WA SARATANI MBALI MBALI KATIKA VIWANJA VYA AZIMIO MJINI ARUSHA

Mapema Leo Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa kushirikiana na Chama cha madaktari Tanzania, wamefanya uchunguzi mkubwa wa Saratani mbali mbali katika viwanja vya Azimio mjini Arusha ambapo imeanza kufanyika kuanzia leo tarehe 24 mpaka 28 mwezi wa 9 mwaka huu.

Akizungumza katika kampeni hiyo ya upimaji, Dr. Kandali amesema kuwa ingawa Leo ni siku ya kwanza, lakini watu wamejitokeza kwa wingi mno kama ilivyo kawaida kwa mikoa mingine ambayo Taasisi ya Saratani Ocean Road huenda kufanya vipimo hivyo, ambapo wakina mama wamejitokeza kwa wingi zaidi ya kina baba.

Kwa upande wa wananchi waliojitokeza kwenye uchunguzi huo, mwananchi mmoja (mwanaume) ambae hakupenda Jina lake litajwe amesema kuwa, wakina baba wengi wameshindwa kujitokeza pengine ni kwakuwa Leo ndio siku ya mwanzo, na ukilinganisha kuwa Leo ni mwisho wa wiki, wengi huamua kubaki nyumbani na familia zao, ingawa alisema kuwa pengine kesho watajitokeza wengi  baada ya kupata maelezo kutoka kwa wenzao ambao watapata huduma Leo.

Taasisi ya Saratani Ocean Road imekuwa ikifanya uchunguzi wa Saratani tofauti kama 

 Matiti, Tezi Dume, Mlango wa kizazi na nyingine nyingi, kwenye mikoa mbalimbali ambapo imekuwa ikipata mafanikio makubwa sana hasa ukizingatia kuwa vipimo vingi hutolewa Bure kabisa

Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa walimbatana na Balozi wa India nchini Tanzania

      Comments Off on

Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa walimbatana na Balozi wa India nchini Tanzania

Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa walimbatana na Balozi wa India nchini Tanzania pamoja na wawakilishi wa kutoka Hospitali mbalimbali nchini India mapema leo wametembelea katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road na kujionea namna shughuli zilivyofanyika katika kufikia malengo waliyojiwekea.

Akizungumza wakati anawasilisha andiko la namna ambavyo Taasisi hii imefanya katika utoaji huduma zake, mkurugenzi mtendaji wa Taasisi hiyo amesema kuwa serikali ya Tanzania inajotahidi vya kutosha kutoa vifaa mbalimbali ambapo hata uwiano wa upimaji kwa wananchi kwa kiasi umeongezeka kutokana na kuimarishwa kwa shughuli za kimaabara ingawa pamoja na yote hayo bado

Taasisi inahitaji kuwekeza zaidi ili kiweza kufikia malengo ya kufikia watu wengi zaidi Tanzania na Nchi za njeUmoja wa nchi za kiarabu pamoja na nchi ya India kwa pamoja wanatembelea hospitali na taasisi kadhaa kuweza kupata changamoto na kuona namna gani wanaweza kuzitatua changamoto hizo ili kuweza kutoa matibabu yenye hadhi ya kimataifa.Aidha muungano huo umekubaliana kuwekeza kwa pamoja kwenye sekta ya Afya ili kuweza kuisaidia serikali ya Tanzania kwa kuokoa pesa nyingi ambazo hutumika katika kusaidia wananchi wake kwenda kutafuta matibabu zaidi nje ya nchi.

Ilala Afya Center kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani Ocean Road wameendelea kutoa huduma mbalimbali za Afya

      Comments Off on

Ilala Afya Center kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani Ocean Road wameendelea kutoa huduma mbalimbali za Afya

Ilala Afya Center kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani Ocean Road wameendelea kutoa huduma mbalimbali za Afya ikiwamo kupima Saratani mbalimbali katika Hospitali ya wilaya ya wete ndani ya visiwa vya Pemba.


Akizungumza mapema leo Daktari kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dr. Katanga amesema kuwa leo ikiwa ni siku ya pili watu wameendelea kujitokeza kwa wingi kupata huduma mbalimbali za kimatibabu kama upimaji wa Macho, masikio na magonjwa mengine mbalimbali huku upimaji wa Saratani ukishika kasi kubwa kwa kupatikana kwa watu wengi.


Aidha Dr. Katanga ametanabaisha kuwa pamoja na kujitoleza kwa watu wengi katika kampeni hiyo, lakini bado amewasihi wananchi wakaazi wa eneo hilo na walioko pembezoni kuendelea kujitokeza kwani muda bado upo sababu kampeni hii inafanyika kuanzia tarehe10 Agosti mpaka Tarehe 13 Agosti mwaka huu.
Nao wananchi wameishukuru Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa kushirikiana na Ilala Afya center kwa kuweza kuunganisha nguvu ili kuleta matibabu sahihi na mengi kwa ujumla wake kwani mtu akifika hapo anapata vipimo vyote na matibabu yote kwa mpigo na akiondoka anakuwa na uhakika na Afya yake.