Mapema Leo Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa kushirikiana na Chama cha madaktari Tanzania, wamefanya uchunguzi mkubwa wa Saratani mbali mbali katika viwanja vya Azimio mjini Arusha ambapo imeanza kufanyika kuanzia leo tarehe 24 mpaka 28 mwezi wa 9 mwaka huu.
Akizungumza katika kampeni hiyo ya upimaji, Dr. Kandali amesema kuwa ingawa Leo ni siku ya kwanza, lakini watu wamejitokeza kwa wingi mno kama ilivyo kawaida kwa mikoa mingine ambayo Taasisi ya Saratani Ocean Road huenda kufanya vipimo hivyo, ambapo wakina mama wamejitokeza kwa wingi zaidi ya kina baba.
Kwa upande wa wananchi waliojitokeza kwenye uchunguzi huo, mwananchi mmoja (mwanaume) ambae hakupenda Jina lake litajwe amesema kuwa, wakina baba wengi wameshindwa kujitokeza pengine ni kwakuwa Leo ndio siku ya mwanzo, na ukilinganisha kuwa Leo ni mwisho wa wiki, wengi huamua kubaki nyumbani na familia zao, ingawa alisema kuwa pengine kesho watajitokeza wengi baada ya kupata maelezo kutoka kwa wenzao ambao watapata huduma Leo.
Taasisi ya Saratani Ocean Road imekuwa ikifanya uchunguzi wa Saratani tofauti kama
Matiti, Tezi Dume, Mlango wa kizazi na nyingine nyingi, kwenye mikoa mbalimbali ambapo imekuwa ikipata mafanikio makubwa sana hasa ukizingatia kuwa vipimo vingi hutolewa Bure kabisa