ZOEZI LA TATHIMINI YA KUKINGA NA KUTHIBITI MAAMBUKIZI YA MAGONJWA (IPC)

      Comments Off on

ZOEZI LA TATHIMINI YA KUKINGA NA KUTHIBITI MAAMBUKIZI YA MAGONJWA (IPC)

Kitengo Cha kuboresha huduma Cha Wizara ya Afya pamoja na Timu ya Taasisi ya Saratani Ocean Road ikiwa tayari kabisa kuanza zoezi la tathimini ya kukinga na kuthibiti maambukizi ya magonjwa (IPC), baada ya kupata baraka zote kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage.

Aidha Dkt. Mwaiselage ameitaka timu ya ORCI kuwa tayari kupokea tathimini hiyo kutoka kwa wakaguzi hao wa Wizara ya Afya, na kuweza kuifanyia kazi katika kuboreshq mapungufu yoyote yale ambayo yanaweza kujitokeza.

Kwa upande wa wakaguzi kutoka wizara ya Afya wanasema kuwa tathimini hiyo ya IPC itakuwa katika viwango vya Kimataifa, hivyo kuongeza ufanisi kwenye utendaji kazi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road huku lengo la tathimini ni kuona kama kuna mapungufu katika sehemu za kutolea huduma, kama zitakuwepo ili zifanyiwe kazi na kuendelea kuboresha katika maeneo yale yatakayokuwa yanafanya vizuri.

Zoezi hilo ambalo litakuwa ni maalum kwaajili ya mustakabali wa maendeleo ya Taasisi yetu, linakadiriwa kuchukua muda wa zaidi ya siku tano.

WATUMISHI WA SHIRIKA LA UWAKALA WA MELI TANZANIA(TASAC) WAFANYIWA UCHUNGUZI WA SARATANI

      Comments Off on

WATUMISHI WA SHIRIKA LA UWAKALA WA MELI TANZANIA(TASAC) WAFANYIWA UCHUNGUZI WA SARATANI

Taasisi ya Saratani Ocean Road leo imeendeleza jukumu lake la kuwafanyia uchunguzi wa Saratani baadhi ya watumishi wa serikali ambapo safari hii watumishi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), wamefanyiwa uchunguzi mwishoni mwa wiki hii.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Bi. Beatrice Mushi, amesema, watumishi wa TASAC wametupa hamasa kubwa sana kwani wamejitokeza kwa wingi kuchunguzwa afya zao.

Taasisi ya Saratani imewafanyia uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa kizazi, Saratani ya Matiti, Saratani ya tezi dume pia na kuwafanyia kipimo Cha HIV pamoja na kipimo Cha Sukari.

Aidha Bi. Beatrice Mushi ametoa wito kwa Taasisi na mashirika mbalimbali ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali wajitokeze katika kufanya uchunguzi wa Afya zao ikiwemo uchunguzi wa maradhi ya Saratani sababu Saratani ikigundulika mapema inatibika.

“Natoa wito kwa mashirika mengine ya kiserikali na yale yasiyo ya kiserikali kuhakikisha kuwa wanafika katika Taasisi ya Saratani Ocean Road kufanya uchunguzi ili kuweza kupata matibabu mapema sababu Saratani ikigundulika mapema inatibika” Alimaliza Bi. Beatrice

SIKU YA SARATANI DUNIANI (4 Feb, 2023)

      Comments Off on

SIKU YA SARATANI DUNIANI (4 Feb, 2023)

Mambo makubwa manne kwa siku ya leo toka kwa mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. JuliusMwaiselage.

  1. Shukrani kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha matibabu kwa kutuletea vifaa tiba vya kutosha kwaajili ya watanzania.
  2. Bima ya Afya kwa wote itasaidia wananchi kuweza kupata matibabu kwa urahisi, hivyo pindi itakapopitishwa tu tuharakishe kujiunga ili kuokoa maisha ya watanzania hasa wa hali ya chini
  1. Siku ya kuadhimisha mapambano dhidi ya Saratani, watanzania wahakikishe wanapata taarifa sahihi kuhusu Saratani.
  2. Shukrani kwa CRDB kwa kutusaidia kuhusu kupata kituo cha mawasiliano cha hudu.a kwa mteja, hii itasaidia kutoa taarifa sahihi kwa watanzania kuhusu huduma zetu za saratani.

CHAMA CHA WANAFUNZI CHA WAFAMASIA TANZANIA (TAPSA) CHAPTER YA MUHAS, JANA MAPEMA WAMEZINDUA KAMPENI YA UELIMISHAJI KUHUSU KANSA YA MLANGO WA KIZAZI

      Comments Off on

CHAMA CHA WANAFUNZI CHA WAFAMASIA TANZANIA (TAPSA) CHAPTER YA MUHAS, JANA MAPEMA WAMEZINDUA KAMPENI YA UELIMISHAJI KUHUSU KANSA YA MLANGO WA KIZAZI

Chama cha wanafunzi cha wafamasia Tanzania (TAPSA) chapter ya MUHAS, jana mapema wamezindua kampeni ya uelimishaji kuhusu kansa ya mlango wa kizazi. Katika warsha hiyo ambayo wameuzulia wanafunzi mbalimbali kutoka katika vyuo tofauti vya wafamasia.

Dkt. Kandali Samweli wa Taasisi ya Saratani Ocean Road katika warsha hiyo ya uzinduzi wa kampeni ya uelimishaji kuhusu kansa ya mlango wakizazi amesema, Saratani ya Mlango wakizazi inashika nafasi ya nne Duniani, lakini kwa Tanzania saratani hii inaongoza kwa kushika nafasi ya kwanza.

Dkt.Kandali amesema kuwa katika mapambano ya Saratani hii, Mambo muhimu ya kufanyia kazi ni kujikita katika kufanya uchunguzi wa mara kwa mara na kuwapatia kinga mabinti. Hususani Kinga ambayo hivi karibuni itazinduliwa kwa ajili ya mabinti wenye umri wa miaka 15 mpaka 26.

Aidha Dkt. Kandali amesisitiza kuwa katika kufanya uchunguzi, kama tatizo likigundulika mapema, nafasi ya kupona ni kubwa zaidi kwa kupatiwa matibabu sahihi.

Ata hivyo Dkt. Kandali amesema kuwa, kutokana sababu mbalimbali zinazosababisha Saratani hii, ngono isiyo salama bado inasimama katika nafasi kubwa ya kupata kirusi hicho Cha Papilloma chenye kuleta Saratani hii ya Mlango wa kizazi.

Hata hivyo Dkt. amesisitiza kuwa Dalili za saratani ya Mlango wa kizazi za awali zipo kimya. Kufanya uchunguzi ndio njia pekee ya kuona hizo Dalili za awali zipo au hazipo. Kama zipo unatibiwa kabla ya Saratani kuanza.

Dkt. Kandali amewaasa wanafunzi wawe mabalozi katika kuwafikishia habari hizi watanzania kuwa uchunguzi unaokoa maisha na Saratani inatibika.

Aidha Mtaalamu wa Tiba mionzi Polikalipo Kagina wa Taasisi ya Saratani Ocean Road amewatoa hofu wanafunzi, kuwa mionzi ni salama kwa kuwa inatumika kwa kiwango maalumu pale palipoathirika tu. Na Tiba mionzi haipunguzi siku ya kuishi.
Kagina ameeleza kuwa, mpaka mgonjwa kuanza kupata Tiba ya mionzi huwa anapitiwa na wataalamu Saba mpaka nane ndipo maamuzi ya Tiba mionzi yanafanyika kwa mgonjwa. Na kila mgonjwa ana kiwango chake Cha mionzi kutokana na tatizo lake.

Halikadhalika Mashujaa wa Saratani ya Mlango wa kizazi Bi Asha Juto na Bi Catherine Bachoo kwa pamoja wamesema kuwa wamepona Saratani na wanaendelea na maisha yao Kama kawaida. Na wamekuwa wakitoa Elimu kuhusiana na Saratani hii ya Mlango wa kizazi.

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA ATEMBELEA WAGONJWA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD NA KUTOA ZAWADI ZA SIKUKUU KWA WAGONJWA

      Comments Off on

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA ATEMBELEA WAGONJWA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD NA KUTOA ZAWADI ZA SIKUKUU KWA WAGONJWA

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi ametembelea wagonjwa wa Taasisi ya Saratani Ocean Road ili kuwajulia hali na kutoa misaada ya sikukuu pamoja na familia yake.

Akizungumza mapema leo alipotembelea wagonjwa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road, Prof. Makubi amesema kuwa ili kutilia mkazo jitihada hizo, serikali tayari imekwishaanza ujenzi wa vituo vingine katika katika Hospitali Kanda ya Rufaa Mbeya,KCMC Kilimanjaro, Bugando Mwanza na Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma.

Prof. Makubi amewapa zawadi mbalimbali pamoja na kunywa nao Chai kama kielelezo cha kuwatia moyo na kuwatakia ahueni kwenye matatizo yanayowasumbua. Aidha aliwafahamisha ya kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan anafahamu changamoto za wagonjwa wa Saratani nchini hivyo anaendelea kusimamia maboresho katika Sekta ya Afya katika kutoa elimu kwa jamii, kubaini mapema, kutibu na kuimarisha Tiba Shufaa Kwa wagonjwa wa Saratani nchini Tanzania

Baadhi ya wagonjwa waliolazwa waliopo kwenye wodi wamemshukuru Prof.Makubi aliyeambatana na Familia yake na pia Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Prof Paschal Ruggajo kwa kuungana nao kwenye chai na kuwa kitendo cha kuwajali na wamefarijika sana leo kwa ziara yake hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. Julius Mwaiselage alielezea maboresho mbalimbali yaliyofanyika katika Taasisi hiyo kwa kusimamiwa na Serikali ya Awamu ya 6 inayosimamiwa na Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan ikiwemo kujenga majengo na kufunga mashine kisasa za Cyclotron, PET/CT Scan, MRI, na ICU. Aidha alisema ya kwamba dawa zote za tiba saratani zinapatikana kwa asilimia 98 na kushukuru Serikali kupeleka fedha MSD ili kununua dawa hizo.

Akizungumzia maandalizi ya kufungua kitengo cha upasuaji (surgical oncology) Dkt. Mwaiselage amesema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na yenye lengo la kuhakikisha huduma nyingi Kwa wagonjwa wa Saratani zinapatikani “chini ya paa moja” la hospitali hiyo.

WIZARA YA AFYA , ELIMU NA FEDHA WASHIRIKIANA KUBUNI UWEKEZAJI NA UPANUZI WA HUDUMA ZA SARATANI NCHINI

      Comments Off on

WIZARA YA AFYA , ELIMU NA FEDHA WASHIRIKIANA KUBUNI UWEKEZAJI NA UPANUZI WA HUDUMA ZA SARATANI NCHINI

Katibu Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi amesema kuwa Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Saratani wamejipanga kushirikiana na sekta zingine hasa Wizara ya Elimu na Fedha nchini ili kuwekeza na kupanua huduma za Saratani nchini.

Prof. Makubi ametoa kauli hiyo leo Jijini Dodoma katika kikao kazi kilichoshirikisha sekta hizo ili kupitia andiko la ufadhili wa uwekezaji na upanuzi wa Huduma za Saratani nchini. Wizara ya Afya kwa sasa ipo katika mkakati ya kushusha huduma za Saratani katika ngazi ya Kanda na mikoa pia kuvutia utalii tiba kutoka nchi za jirani.

Prof. Makubi ametoa wito kwa sekta zote tatu kuwa na ushirikiano wa kisekta katika kuratibu utafutaji wa ufadhili wa fedha za kutekeleza mradi wa kusogeza huduma za Saratani katika hospital za rufaa za kanda na mikoa. 

Andiko la upanuzi wa huduma za saratani nchini linagharimu shilingi za Kitanzania billioni 240 kwa ajili ya miundombinu, vifaa, watalamu, mafunzo na kinga na inategemewa Serikali itasaidiana na wadau mbalimbali na sekta binafisi katika kufanikisha uwekezaji huo. 

Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mukajungu Kamuzora amesema wako tayari kushirikiana kutafuta wafadhili ili kufanikisha upatikanaji wa huduma hizo karibu na wananchi.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dkt. Julius Mwaisalage ameishukuru Serikali na kusema kuwa iwapo andiko ilo litapita na kutekelezwa kikamilifu itasaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa wa saratani katika Hospitali ya Ocean Road kwani huduma za kibingwa zitakuwa zimesogezwa karibu na wananchi

ON 12TH DECEMBER 2022, A HEALTH MEETING WAS CONVENED TO DISCUSS POSSIBLE COLLABORATION BETWEEN TANZANIA AND HEALTH STAKEHOLDERS FROM THE UNITED STATES ON THE ESTABLISHMENT OF CENTRE OF EXCELLENCE ON ONCOLOGY IN TANZANIA

      Comments Off on

ON 12TH DECEMBER 2022, A HEALTH MEETING WAS CONVENED TO DISCUSS POSSIBLE COLLABORATION BETWEEN TANZANIA AND HEALTH STAKEHOLDERS FROM THE UNITED STATES ON THE ESTABLISHMENT OF CENTRE OF EXCELLENCE ON ONCOLOGY IN TANZANIA

On 12th December 2022, a health meeting was convened to discuss possible collaboration between Tanzania and health stakeholders from the United States on the establishment of Centre of Excellence on Oncology in Tanzania. The meeting was organized by the Embassy of the United Republic of Tanzania in Washington D.C in collaboration with Global Health Catalyst. Hon. Dr. Godwin Mollel (MP), Deputy Minister of Health was the guest of honor. The event was held at the Embassy of Tanzania in Washington D.C.


The event brought together a total of 36 participants from pharmaceutical companies, manufacturers of diagnostic and treatment equipment, health systems organizations, research and training institutions, public education and advocacy organizations. Special presence was a representative from the White House, Dr. Catherine Young, Senior Director of Policy for the President Biden Cancer. The health companies that were attended includes, Pfizer, Bristal Myers Squibb, Sister Cities International, Texas Children Hospital – Global Hope, BVGH, Global Health Catalyst, Bayer, John Hopkins University, University of Pennsylvania, GE Healthcare, Nanocan Therapeutics, Bayer, Varian, BMS, Siemens, Abbott, and Lancet Oncology.
In his remarks, Hon. Dr. Godwin Mollel (MP), Deputy Minister of Health ensured the participants of Tanzania’s readiness to support the establishment of Centre of Excellency. He further invited the companies to consider establishing medicine and medical devices plants in Tanzania to take advantage of the ready local and regional market.


Participants were committed to assist Tanzania in the fight against cancer through the establishment of the Center of Excellence for a coordinated efforts in preventive programs, screening and diagnosis, availability of medicines, treatment options including state-of-the-art proton therapy, collaborative research, and training of experts for cancer care. A seed fund in a tune of USD 5 Million is allocated for establishment of the center starting in early 2023.
Sum up remarks were given by the Moderator, Prof Wil Ngwa of John Hopkins University and Director of Global Health Catalyst. The closing remarks were given by Dr Julius Mwaiselage, Executive Director of Ocean Road Cancer Institute. The resolution of the meeting was to form a working team which will ensure a continued discussion between Tanzania and USA to make the initiative a reality; developing MOUs to foster collaboration in trainings and research which can start as early as possible, and a visit to Tanzania by the Global Health Catalyst in 2023 in order to progress the plans to establish the center.

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA DKT. SEIF SHEKALAGHE AMESEMA KUWA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD INATAKIWA IJIKITE KATIKA TAFITI ZA SARATANI PAMOJA NA KUTOA ELIMU YA UELEWA WA SARATANI KWA JAMII

      Comments Off on

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA DKT. SEIF SHEKALAGHE AMESEMA KUWA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD INATAKIWA IJIKITE KATIKA TAFITI ZA SARATANI PAMOJA NA KUTOA ELIMU YA UELEWA WA SARATANI KWA JAMII

Naibu katibu mkuu wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe amesema kuwa Taasisi ya Saratani Ocean Road inatakiwa ijikite katika Tafiti za Saratani pamoja na kutoa Elimu ya kutosha kwa jamii ili uwelewa uwe mkubwa jambo litakalopelekea kupungua kwa Maradhi ya Saratani.

Dkt. Shekalaghe ameyasema hayo mapema jana alipotembelea katika Taasisi hii ili kuweza kujionea namna huduma zinavyotolewa na pia kujionea mashine zinavyofanya kazi.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage amesema kuwa, wamepokea maelekezo hayo tayari kwa kuyafanyia kazi huku akisisitiza kuwa wataendelea kutoa huduma pamoja na kusimamia baadhi ya vituo vya Afya kama vile
Mtwara na Kigoma ambavyo kwasasa vipo chini ya Taasisi hii.

Akiendelea kwenye taarifa yake Dkt. Mwaiselage amesema kuwa Taasisi itajikita pia kwenye Tafiti za kibingwa pamoja na kuongeza Elimu kwa umma pamoja na kutoa Kinga kwa jamii ili kupunguza idadi ya watu watakaoathirika na ugonjwa huu huku wakiedelea kufanya ufatiliaji wa huduma zote za saratani zinazotolewa katika hospitali nyingine.

UJENZI ICU YA KISASA WAFIKIA 99%, MRI 100% HUDUMA ZA TIBA ZAZIDI KUMAILIKA KATIKA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD(ORCI)

      Comments Off on

UJENZI ICU YA KISASA WAFIKIA 99%, MRI 100% HUDUMA ZA TIBA ZAZIDI KUMAILIKA KATIKA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD(ORCI)

Bodi ya wadhamini katika Taasisi ya Saratani Ocean Road leo majira ya asubuhi wametembelea Miradi kadhaa inayotekelezwa kupitia fedha za IMF katika Taasisi hiyo.

Akizungumza wakati anatoa taarifa fupi kuhusu mradi wa ICU, mratibu wa Miradi ya IMF katika Taasisi hiyo ndg Mohammed Mbwana, amesema kuwa, mradi huo utakaochukua zaidi ya wagonjwa mahututi 24 umegharimu jumla ya kiasi cha shilingi milioni 800 mpaka kumalizika kwake.

Wakati huohuo Bw. Mbwana amesema kuwa mradi huu umetekelezwa kwa kufata taratibu zote za kimanunuzi na kwamba hakuna mwanya wowota uliotumika kupitish pesa kwa utaratibu au matumizi mengine tofauti na iliyokusufiwa.

Nae mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage amewaeleza wajumbe wa bodi kwamba thamani ya fedha imesimamiwa katika ujenzi na vifaa ambavyo vina mkataba matengenezo kinga ya miaka mitano

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi hiyo ya wadhamini Prof Ephata Kaaya amewapongeza uogozi wa Taasisi hiyo kwa kuweza kusimamia jengo hilo, ambapo litakuwa tayari kwaajili ya matumizi punde tu vifàa vingine vitakapomaliziwa kufungwa.