MADAKTARI KUTOKA NCHINI INDIA “TATA MEMORIAL HOSPITAL” WATEMBELEA ORCI

      Comments Off on

MADAKTARI KUTOKA NCHINI INDIA “TATA MEMORIAL HOSPITAL” WATEMBELEA ORCI

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Dkt. Julius Mwaiselage leo amekutana na madaktari kutoka nchini India wa “Tata memorial Hospital”

Dkt. Mwaiselage amewaelezea namna Taasisi ya Saratani Ocean Road inavyofanya majukumu yake katika kuwahudumia wagonjwa wa Saratani.

Pamoja na hayo Dkt. Mwaiselage amewaambia kuwa milango ipo wazi ya kushirikiana baina ya Taasisi ya Saratani Ocean Road na Tata Memorial Hospital katika nyanja za utafiti, matibabu na sehemu nyingine katika maswala ya saratani.

Aidha madaktari hao kutoka Tata Memorial Hospital wamepata fursa ya kufanya ziara katika moja ya maabara za Taasisi ya Saratani Ocean Road, mashine ya Tiba mionzi ya Colbat, kwenye tiba kemia pamoja kwenye jengo la Pet na Cyclotron.

Madaktari hao kutoka Tata Memorial Hospital wamesema wao wapi tayari kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani Ocean kutegemea na mahitaji ya Taasisi yatakavyokuwa.

WAZIRI WA AFYA MH. JENISTA MHAGAMA LEO AMETEMBELE KATIKA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD

      Comments Off on

WAZIRI WA AFYA MH. JENISTA MHAGAMA LEO AMETEMBELE KATIKA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD

Waziri wa afya Mh. Jenista Mhagama leo ametembele katika Taasisi ya Saratani Ocean Road kuona huduma za Tiba mionzi zinavyoendelea katika Taasisi hiyo.

Mh. Mhagama amejionea mashine za Linac na Colbat ambazo zinatumika katika kutoa huduma ya Tiba mionzi kwa wagonjwa wa Saratani.

Ikiwa Taasisi ya saratani Ocean Road Ina mashine mbili za Linac na moja kati ya hizo bado inahitilafu.

Aidha Mhe. Mhagama amesema wakati akizungumza na wananchi waliokuwa wanasubili matibabu amesema serikali ipo mbioni kuongeza mashine nyingine ya Tiba mionzi ili kuondoa shida zinazotokana kwa kuharibika kwa mashine.

Aidha upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage ameishukuru serikali kwa kufanya mchakato wa kuongeza mashine nyingine ya Tiba mionzi itakayokuja hivi karibuni.

TIBA SHUFAA KUINGIZWA KATIKA MTAALA WA MAFUNZO YA AFYA NCHINI

      Comments Off on

TIBA SHUFAA KUINGIZWA KATIKA MTAALA WA MAFUNZO YA AFYA NCHINI

“Tiba shufaa kuingizwa katika mtaala wa mafunzo ya afya nchini”, hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za utengemao, Tiba shufaa na wazee kutoka wizara ya afya Dkt. Mwinyikondo Amir kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama katika maadhimisho ya siku ya Tiba shufaa Duniani.

Maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Taasisi ya Saratani Ocean Road jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya nchini.

Dkt. Mwinyikondo kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Mhagama amesema wizara ya afya ipo katika mchakato maalum wa kuingiza Tiba shufaa katika mtaala wa mafunzo ya afya nchini.

Ameendelea kusema serikali inawashukuru wadau mbalimbali wa Tiba shufaa nchini kwa kuwapa mafunzo watumishi wa afya ili kuongeza wataalamu wa Tiba shufaa nchini.

Tiba shufaa hutolewa kwa ushirikiano shirikishi wa wataalamu wenye taaluma mbalimbali wakiwemo madaktari, wafamasia, wauguzi, maafisa ustawi wa jamii pia wataalamu wa saikolojia, wataalamu wa magonjwa ya akili, wataalamu wa lishe, viongozi wa dini na wengine kutokana na uhitaji wa mgonjwa.

Dkt. Mwinyikondo ameipongeza Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa kuanza kuwatembelea wagonjwa na kuwapelekea huduma pale walipo hasa majumbani.

Huduma hiyo ya majumbani ni kitendo ambacho itasaidia sana kupunguza idadi ya wagonjwa mahospitalini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Julius Mwaiselage amesema karibia asilimia themanini ya wagonjwa wa Saratani wanaitaji huduma ya Tiba shufaa.

Na Taasisi ya Saratani Ocean Road imejikita katika kuimarisha huduma za Tiba shufaa zinazotolewa katika Taasisi na majumbani.

Pamoja na hayo Dkt. Mwaiselage amesema upatikanaji wa dawa ya Morphine ni asilimia miamoja zinapatika katika Taasisi.

MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA WA SARATANI

      Comments Off on

MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA WA SARATANI

Wito umetolewa kuongeza nguvu katika kuelimisha jamii ili kuongeza mashujaa wa Saratani na kuleta matumaini zaidi kwa wagonjwa.

Akizungumza na mashujaa pamoja na wadau mbalimbali wa Afya katika maadhimisho ya siku ya mashujaa Duniani leo tarehe 2 Juni 2024, Mkurugenzi msaidizi wa magonjwa yasiyoambukiza kutoka wizara ya Afya Dkt. Omari ubuguyu ambae pia ndie aliyekuwa mgeni Rasmi amesisitiza kuwekeza kwenye utoaji wa elimu kwani ndio njia pekee itakayosaidia kupunguza kasi ya ugonjwa huu.

Aidha Dkt. Ubuguyu amesema kuwa Sera ya afya ina vipengele vya kutoa misamaha kwa wagonjwa wasio na uwezo na serikali inafanya hivyo kupitia Taasisi zake kama hii Taasisi ya Saratani Ocean Road husamehe pia ingawa amesisitiza kuwa kwa wale wenye uwezo inabidi wachangie ili kufanya shughuli ya utoaji huduma kuwa nyepesi na kuongeza wigo wa kusaidia watu wengi zaidi wasio na uwezo.

Nae Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt Julius Mwaiselage amesema kuwa kwasasa huwa wanatoa misamaha hadi Bilioni mbili kwa mwezi lengo likiwa ni kila atakaefika katika Taasisi hii awe na uwezo au hata asiwe na uwezo, apate huduma ya matibabu.

Katika hatua nyingine Dkt. Mwaiselage ameihabarisha jamii kuwa ufungwaji wa mashine ya PET-CT Scan upo tayari na matumizi yake yataanza mapema mwezi huu wa sita kwani tayari majaribio ya matumizi yake yamekwishafanyika na kufanikiwa kwa asilimia Mia moja.

Dkt. Mwaiselage amesema huduma ya upasuaji kwa sasa itakuwa ikifanyika hapa hapa katika Taasisi hii kuanzia mwezi wa nane mwaka huu wa 2024, kwani marekebisho madogo madogo yanaendelea.

Dkt. Mwaiselage amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kupatikana kwa mashine stahiki pamoja na ujenzi na ukarabati wa majengo kwaajili ya huduma hizo.

Nae mkurugenzi wa Shujaa Cancer Foundation Bi Gloria Kida amewashukuru Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa kutoa ushirikiano mkubwa kwao kwenye maandalizi ya shughuli hii.

TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD YASHINDA MASHINDANO MEI MOSI TAIFA 2024 YALIYOFANYIKA JIJINI ARUSHA

      Comments Off on

TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD YASHINDA MASHINDANO MEI MOSI TAIFA 2024 YALIYOFANYIKA JIJINI ARUSHA

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya saratani Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage amepokea vikombe vya ushindi vya Taasisi ya saratani Ocean Road katika mashimdano ya Mei Mosi Taifa 2024 yaliyofanyika mkoani Arusha.

Taasisi ya saratani Ocean Road imekuwa mshindi wa Kwanza katika mchezo wa bao kwa wanaume, huku ikishika nafasi ya tatu kwa wanaume kwenye mbio za baiskeli.

Dkt. Mwaiselage amewapongeza washiriki wote walio iwakilisha Taasisi katika mashindano hayo ya Mei Mosi huku akisema kuwa Taasisi ya Saratani ni kubwa na imebarikiwa kiasi kwamba pamoja na kutoa huduma za matibabu ya Saratani, wanashiriki na kushinda katika michezo mbalimbali.

Wakati huo huo Dkt. Mwaiselage kipekee amewapongeza mshindi wa Kwanza wa Bao Bw. Moshi Mteta na mshindi wa tatu wa mbio za Baiskeli Bw. Stephen Sanga, huku akisisitiza wengine kuongeza juhudi ili wakati ujao tupate makombe mengi zaidi.

Dkt. Mwaiselage amesisitiza ushiriki wa mazoezi kila jumamosi kama ishara ya kuunga mkono agizo la waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa lakini pia kujiweka katika hali ya kuepukana na athari za magonjwa yasiyoambukizwa.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA AFYA NA MASUALÀ YA UKIMWI IMETEMBELEA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD MAPEMA LEO 23/02/2024

      Comments Off on

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA AFYA NA MASUALÀ YA UKIMWI IMETEMBELEA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD MAPEMA LEO 23/02/2024

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI imetembelea Taasisi ya Saratani Ocean Road mapema leo tarehe 23/02/2024

ili kujionea utoaji wa huduma na miradi mbalimbali iliyopo katika Taasisi hiyo.

Kamati hiyo ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti, Mhe Dkt. Faustine Ndungulile wameipongeza Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa kuweza kuisimamia miradi inayotekelezwa kwa fedha nyingi kwa ustadi wa hali ya juu.

Miradi hiyo ikiwemo mradi mpya wa PET/CT Scan na Cyclotron ambao umeghalimu zaidi ya kiasi cha Shilingi bilioni 18, na upo tayari kwa kuanza kutumika mapema iwezekanavyo.

Miradi mingine ni wa mashine ya MRI, CT- Scan, na ujenzi wa jengo la Multipurpose Oncology.

Pamoja na hayo Dkt. Ndungulile ametoa pongezi kwa huduma bora na za kipekee zinazotolewa katika Taasisi hiyo ikiwemo misamaha ya takribani Tshs 2.2 bilioni kila mwezi hasa ukizingatia kuwa wengi wa watanzania hawana uwezo wa kujihudumia kutokana na maradhi hayo.

Aidha kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Mhe Dkt. Godwin Mollel amesema Serikali inaongeza jitihada za kupeleka huduma za saratani katika hospitali za kanda ili kuipunguzia mzigo Taasisi na tayari kanda zote zinahuduma ya tiba saratani; na kuongeza ya kwamba Wizara imeiagiza Ocean Road kujenga kituo cha saratani Mbeya na ujenzi utaanza katibuni. Aidha, amesema kwambw Wizara imepokea maelekezo na ushauri wa Kamati na itayafanyia kazi kwa ustawi wa sekta ya afya nchini.

Awali Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage akiwasilisha ripoti alieleza mafanikio mengi ya utoaji huduma za kinga, uchunguzi, tiba, mafunzo na utafiti pamoja na changamoto zilizopo katika Taasisi zinapungua kadiri muda unavyokwenda kwa kuwa serikali inatoa mchango mkubwa katika kukabiliana na changamoto hizo.

SERIKALI IMETOA RAI KWA JAMII KUCHUKUA HATUA ZA MAPEMA KUPIMA UGONJWA WA SARATANI

      Comments Off on

SERIKALI IMETOA RAI KWA JAMII KUCHUKUA HATUA ZA MAPEMA KUPIMA UGONJWA WA SARATANI

SERIKALI imetoa rai kwa jamii kuchukua hatua za mapema kupima ugonjwa wa saratani, kufanya mazoezi na kufuata mtindo bora wa maisha, kwani kuna ongezeko kubwa la wagonjwa, huku asilimia kubwa ya waathirika wakiwa ni wanawake.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya saratani duniani kwaniaba ya Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, Mkurugenzi wa Huduma za Afya na Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Rashid Mfaume, amesema hadi kufikia mwaka 2030 athari za saratani zitakua mara mbili zaidi hasa katika nchi zenye kipato cha chini.

Pia amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa uwekezaji mkubwa aliyoufanya katika Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), ambapo ametoa zaidi ya shilingi bilioni 18 za ununuzi wa vifaa tiba.

Alisema kutokana na uwekezaji mkubwa uliyofanyika kuna wagonjwa kutoka Zambia, Comoro , Msumbiji , Burundi na Kenya ambao wanafika ORCI kupata matibabu.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Dk. Julius Mwaisalage, amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa uwekezaji mkubwa anaoendelea kuufanya katika taasisi hiyo, ikiwemo ununuzi wa mashine ya kisasa ya uchunguzi wa saratani.

Alisema saratani inayoongoza ni ya Mlango wa kizazi inafuatiwa na saratani ya matiti.

Dk. Mwaisalage amesema ORCI inaendelea kusimamia utoaji huduma za kibingwa kuanzia kinga na uchunguzi huku akisema, maadhimisho ya siku ya saratani mwaka huu yana kauli mbiu isemayo ‘Saratani inatibika huduma sawa kwa wote’.

Naye Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Dk. Alphoncia Nanai, amesema katika kipindi cha mwaka 2022 kwa ukanda wa Afrika wagonjwa wa saratani walikua ni zaidi ya 800,000, huku takribani 600,000 wakipoteza maisha.

Shughuli hii imeambatana na uzinduzi wa mchezo wa Afya game ambapo kwa shilingi 500 tu utachangia mgonjwa wa Saratani huku ukijiweka katika nafasi ya kushinda pikipiki, Nyumba na simu kibao, mchezo huu umeandaliwa na wamata kwa udhamini wa Infinix

WAZIRI WA AFYA, MHE. UMMY MWALIMU AMEAGIZA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD (ORIC) KUANZA KUTOA MATIBABU YA PET -CT SCAN

      Comments Off on

WAZIRI WA AFYA, MHE. UMMY MWALIMU AMEAGIZA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD (ORIC) KUANZA KUTOA MATIBABU YA PET -CT SCAN

Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu ameagiza Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORIC) kuanza kutoa matibabu ya PET -CT Scan ifikapo Februari Mosi Mwaka huu, kutokana na kukamilisha kwa jengo la kutoa huduma hiyo na kufungiwa mashine hiyo ya mionzi, kwani sababu kubwa ya wagonjwa wengi wa saratani kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Waziri Ummy aliyasema hayo mapema leo alipofanya ziara hapa Taasisi ya Saratani Ocean Road na kukagua jengo jipya litalotumika kutoa huduma za mionzi ikiwemo PET CT, pamoja na Cyclotron.

Aidha waziri Ummy Alisema kuwa wataendelea kuboresha huduma zaidi hususan kujenga wodi nzuri zenye ubora, kuhakikisha wanawavutia watu wa viwango tofauti vya maisha kuja kutibiwa nchini.

Waziri Ummy alisema serikali itaendelea kuwekeza zaidi katika Taasisi hiyo, kuhakikisha inaboresha huduma zake na miundombinu, ili watanzani wapate huduma bora za matibabu ya saratani.

Kuhusu kuanza kwa mashine ya PET CT Scan, aliwataka kuhakikisha wanaanza huduma hizo za matibabu haraka kutokana na kukamilika miundombinu ya kutolea huduma, ambapo atawaomba kiongozi mmoja kuizindua ili kuanza rasmi kutoa huduma kwani ndio sababu kubwa ya wagonjwa hao kwenda nje ya nchi.

Katika hatua nyingine waziri Ummy aliagiza ORCI, kuhakikisha wanaanza kutoa huduma za upasuaji wa saratani ili kuwaepushia usumbufu wagonjwa kuzunguka katika hospitali zingine, wakati wangependa kutibiwa hospitalini hapo na kumaliza kila kitu.

“Mmenambia kila kitu mnacho, chumba kipo mtaalamu mnaye, hivyo hadi kufika Julai Mosi, muwe mmeanza kutoa huduma hii, mana hiyo itakuwa inaakisi dhamira nzima ya Taasisi hii ya saratani na umahiri wake wa kuwa kituo bora cha umahiri wa kutibu saratani na kutokana na uwekezaji mkubwa wa serikali hususani katika mashine za mionzi,” alisema

Alisisitiza kuwa, serikali itaendelea kusikiliza Taasisi hiyo katika kuwajengea uwezo hivyo na wao wahakikishe wanatanua utoaji wa huduma na kuwajengea uwezo wataalamu katika hospitali za Kanda na mikoa.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy, ameipongeza Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa utoaji huduma bora zilizopunguza malalamiko kwa wananchi na kusaidia Watanzania wengi kupitia huduma zinazopatikana katika hospitalini hapo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ORCI, Julius Mwaiselage alimshukuru Waziri Ummy kufanya ziara katika taasisi hiyo huku akimpongeza kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea fedha za ujenzi wa miundombinu.

Alisema kwasasa wanayo mipango mbalimbali ya kujenga jengo jipya katika eneo la tasisi hiyo, huku wakiendelea na mipango ya kuandaa michoro ya ujenzi wa majengo ya kutoa matibabu ya saratani Dodoma na Mbeya.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Dk.Mark Mseti alisema wataendelea kuboresha huduma za matibabu kwa wananchi ikiwemo kutoa msamaha kwa wagonjwa wasio na uwezo.

TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD LEO IMEPOKEA MSAADA WENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 137 KUTOKA KWA KAMPUNI YA GSM

      Comments Off on

TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD LEO IMEPOKEA MSAADA WENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 137 KUTOKA KWA KAMPUNI YA GSM

Taasisi ya Saratani Ocean Road leo imepokea msaada wenye thamani ya Shilingi milioni 137 kutoka kwa mmiliki wa kampuni za GSM Bw. Ghalib Said Mohamed katika kusheherekea siku yake ya kuzaliwa, ambapo pamoja na msaada huo ameshiriki chakula na watumishi wa Taasisi hiyo pamoja na wagonjwa.

Katika sherehe hiyo ambayo imefanyika katika viwanja vya Taasisi ya Saratani Ocean Road, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Albert Chalamila ndiye alikuwa mgeni rasmi ambapo ametoa wito kwa watanzania kutoa sadaka ili kuwasaidia wagonjwa katika mahitaji yao ya matibabu kama ambavyo amefanya leo Bw. Gharib Mohamed.

Aidha Mh. Chalamila amesema kuwa watanzania hatuna budi kumshukuru Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta mashine mbalimbali katika Taasisi hii ikiwemo Pet CT-Scan ambayo itaweza kuchunguza Saratani katika hatua ambazo mashine nyingine hazitaweza huku akisisitiza kuwa muda si mrefu itaanza kufanya kazi katika Taasisi ya Saratani Ocean Road.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage amemshukuru mmiliki wa GSM kwa msaada wake aliotoa wa vifaa hivyo.

Dkt. Mwaiselage amesema vifaa hivyo ikiwemo vile vya Tiba ya Saratani vitasaidia katika huduma mbalimbali kwa wagonjwa wa Taasisi hiyo, huku vikirahisisha utoaji wa huduma hizo kwa jamii ya watanzania na wanaotoka nje ya mipaka ya Tanzania.

MAADHIMISHO YA WIKI YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA

      Comments Off on

MAADHIMISHO YA WIKI YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA

Naibu waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akimsikiliza mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage akizungumza kuhusu huduma zinazotolewa hapa Mnazi mmoja katika banda la Taasisi hiyo.

Leo ndio maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukizwa ambapo Taasisi ya Saratani Ocean Road ipo hapa Mnazi Mmoja ikitoa huduma za uchunguzi wa Saratani za Matiti, Mlango wa kizazi pamoja na Tezi dume bila malipo yoyote, hivyo watu wote wanakaribishwa kufanya uchunguzi huu.

Dkt. Mollel ndie mgeni rasmi wa maadhimisho hayo yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja ambapo amekuja kumuwakilisha waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa kassim Majaliwa.