Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi

      Comments Off on Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi

Baraza la tano la wafanyakazi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road lilizinduliwa tarehe 28/1/2020 katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu. Nyerere uliopo katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Kabla ya kuzinduliwa kwa baraza hilo ulifanyika uchaguzi wa katibu na katibu msaidizi wa Baraza ambapo ndugu Yusuph Fikirini alichaguliwa kuwa katibu na ndugu Joha Kibira kuwa Katibu Msaidizi.

Picha ya pamoja Mgeni Rasmi na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi – ORCI

Picha Mwenyekiti akiwaongoza wajumbe katika uchaguzi wa Katibu wa Baraza

Mwenyekiti akiwatambulisha Katibu na Katibu msaidizi wa Baraza mara baada ya kuchaguliwa.

Mgeni rasmi akishiri kuimba wimbo wa mshikamano daima alipowasili ukumbini

Katibu wa Baraza akitoa utambulisho wa wajumbe wanaounda Baraza kwa Mgeni rasmi

Kabla ya uzinduzi Mwenyekiti wa Baraza ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dr. Julius Mwaiselage, alitoa taarifa ya utendaji ya Taasisi na Baraza lililomaliza muda wake. Kuwa, baraza lilitekeleza wajibu wake kwa kuibua na kujadiliana njia za kuoberesha huduma za Taasisi Pamoja na kuipitia maoteo ya bajeti ili kupata mahitaji halisi ya Taasisi kutoka kila idara.

Mwenyekiti wa Baraza akito hotuba ya utangulizi kabla ya uzinduzi wa Baraza.

Baraza hili lilizinduliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mheshimiwa Dkt. Zainabu Chaula.

Akizindua Baraza Katibu Mkuu katika hotuba yake aliwaagiza na kuwataka wafanyakazi kwa kupitia wajumbe wa baraza kukuhakikisha yafuatayo;

  • Wafanyakazi wawe huru kushauri na Viongozi wakubali kushauriwa
  • Kuzidi kuboresha wamasiliano
  • Kuendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa ikiwa ni pamoja na kuwahurumia na kuwafariji,
  • Kuepuka vitendo vya rushwa
  • Wawakilishi wa baraza wasaidie kuwabadilisha wafanyakazi wengine waweze kufanyakazi vizuri ili kwa pamoja tuweze kutimiza adhi ya Serikali ya Kuboresha afya za wananchi.

Wajumbe wa Baraza wakifiatilia hotuba ya Mgeni Rasmi

Baada ya uzinduzi wajumbe wa baraza walipata mafunzo juu ya uendeshaji wa mabaraza, Utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa mahali pa kazi.

Mwezeshaji akiendelea kuwasilisha mada ya uendeshaji wa mabaraza

Wajumbe wakifuatilia mada inayowasilishwa